Saturday, 6 June 2020

RAIS MAGUFULI AFARIJIKA NA HATUAZA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO KATIKA BENKI YA WALIMU (MWALIMU COMMERCIAL BANK)

...

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Ijumaa Juni 5, 2020
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) wakiwa wamejawa na furaha wakati wa mkutano huo uliofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 5, 2020
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) (Anayemaliza muda wake) Mwalimu Leah Ulaya wakiwapungia mikono wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama hicho wakati Rais akiwasili uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Ijumaa Juni 5, 2020
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Mwalimu, Bw. Richard Makungwa (kulia) akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania (anayemaliza muda wake), Bw. Deus Seif wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa CWT kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Ijumaa Juni 5, 2020
                                                                                 **
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kufarijika kwake kutokana na changamotozilizokuwa zikiihusu benki ya Walimu (Mwalimu Commercial Bank plc) sasa zimeanza kushughulikiwa.

Rais ametoa kauli hiyo Ijumaa Juni 5, 2020 wakati akihutubia mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwenye uwanja wa Jamhuri jijini
Dodoma.
“Najuachama hiki kina mali na rasilimali mbalimbali, lakini zote hizo ni mali za wanachama hivyo basi viongozi hawana budi kuhakikisha mali na rasilimali za wanachama
zinatumika kwa malengo yaliyokusidiwa….Na katika hilo nimefarijika kidogokusikia kuwa baadhi ya changamoto nilizozitaja kwenye mkutano wa chama cha walimu
Tanzania mwaka 2017 zenye kuihusu benki ya Walimu zimeanza kushughulikiwa.”
Alisema Rais Magufuli.
Aliwatakaviongozi watakaochaguliwa kwenye mkutano huo wa Dodoma waendelee kutatua mapungufu mengine yaliyobaki kwenye benki hiyo ili wanachama wake wafaidike
kama ilivyotarajiwa wakati wa kuanzishwa kwake.
Awalikatika risala ya wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi iliyosomwa kwa niaba yao naKatibu Mkuu wa CWT (aliyemaliza muda wake), Mwalimu Deus Seif alisema tangu
walimu wakutane na Rais mwaka 2017 yapo mambo mengi yamefanyika kuhusiana na benki hiyo ambapo kwa upande wa uongozi kwa sasa chama kina wakilishwa na
walimu wanne  katika bodi ya wakurugenzi.
Aidhakwa upande wa mikopo zaidi ya asilimia 90 imetolewa kwa walimu wakati asilimia 5.3 imetolwa kwa wafanyakazi wengine wa serikali.
Vilevile Chama Cha Walimu (CWT) kwa kushirikiana na benki pamoja na PSSSF wataweka utaratibu kwa walimu wastaafu kupokea mafao yao kupitia benki yao ya Mwalimu
Commercial Bank.
“ChamaCha Walimu kwa kushirikiana na benki tumefikia muafaka kufungua tawi jingineDodoma mwishoni mwa mwaka huu ambapo pia benki inaendelea na teknolojia ya
mifumo ya kidijitali ili kufikia walimu wengi katika mikoa mbalimbali nchini.” Alisema Bw. Seif.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger