Monday, 15 June 2020

Mbunge ‘Bwege’ Atangaza Kuhamia ACT Wazalendo

...
Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, Selemani Bungara maarufu kwa jina la Bwege ametangaza kukihama Chama Cha Wananchi Cuf na kuhamia Chama cha ACT Wazalendo mara baada ya bunge kuvunjwa hapo kesho Jumanne Juni 16 2020.

Bugala ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Juni 15, 2020 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam;

“Ninawatangazia rasmi kuwa likivunjwa Bunge tu mimi sio tena mwanachama wa CUF karibuni ACT Wazalendo."-Amesema

Bwege amesema haendi ACT Wazalendo kwa kumfuata Maalim Seif bali amekwenda kwa kuwa chama hicho ni kipya na kina mwelekeo mzuri kisiasa


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger