Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewaagiza Wakuu wa Polisi wa Wilaya OCDs kuhakikisha wanasimamia mikutano wakati wa kampeni ili iwe ya amani na utulivu.
IGP Sirro amesema hayo leo akiwa mkoani Simiyu wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika mkoa huo na kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo ambapo alisema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga kusimamia uchaguzi na kwamba litaendelea kutoa elimu kwa wananchi ikiwa pamoja na kushirikiana ipasavyo na wadau wa uchaguzi.
Aidha, IGP Sirro amewapandisha vyeo askari wawili wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia FFU mkoa wa Simiyu kutoa cheo cha konstebo wa Polisi na kuwa Koplo wa Polisi kutokana na umahili wao wa kutekeleza majukumu wanayopewa.
0 comments:
Post a Comment