Eneo ambalo kiwanda cha LNG kinatarajiwa kujengwa katika kijiji cha Likong’o katika Manispaa ya Lindi
**
Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imeanza kutekeleza zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi ambao wanaguswa na mradi wa uchakataji na usindikaji wa gesi asilia (LNG) Mkoani Lindi.
Mradi huo ambao unagusa Mitaa mitatu ya Likong’o, Masasi ya Leo na Mto Mkavu unachukua eneo lenye ukubwa wa hekta 2,071.7, ambapo Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 5.2 kwa ajili ya kufidia wanachi 693 ambao wanaguswa na mradi huo.
Akizungumzia mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi alisema, “mchakato wa kuwafidia waathirika wa mradi wa LNG umechukua muda mrefu sana na nimekuwa nikijibu maswali mengi sana kutoka kwa wananchi hao.
Hatimaye Serikali imeidhinisha kiasi cha Shilingi Bilioni 5.2 kufidia wananchi wanaoguswa na mradi huu muhimu. Napenda kutumia fursa hii kuishukuru Serikali pamoja na Shirika letu la TPDC kufikia hatua hii muhimu.”
Wananchi watakaopisha mradi wa LNG eneo la Likong’o, Manispaa ya Lindi wakifuatilia na kusmsikiliza kwa makini Afisa Maendeleo ya Jamii Ndugu Oscar Mwakasege kutoka TPDC, alipokuwa akiwasilisha mada ya utatuzi wa migogoro ya wananchi katika mradi huo
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akitoa maelezo ya mradi wa LNG mbele ya Waandishi wa Habari Ofisini kwake.
**
Katika hatua nyingine, Meneja mradi wa LNG kutoka TPDC, Mhandisi Fedister Agrey aliwahakikishia wananchi na vyombo vya habari kwamba, “mradi upo na ndiyo maana kikosi kazi kutoka TPDC, Benki ya NMB pamoja na Taasisi zingine za Serikali wapo hapa.”
“Zoezi hili linatekelezwa katika hatua mbili, hatua ya kwanza inahusisha utoaji wa elimu ya fidia, matumizi sahihi ya fedha, sharia na utatuzi wa migogoro kwa waathirika wote wa mradi.
Na hatua ya pili itahusisha zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi husika” alisisitiza Mhandisi Fedister. Wananchi watakaopisha mradi wa LNG eneo la Likong’o, Manispaa ya Lindi wakifuatilia na kusmsikiliza kwa makini Afisa Maendeleo ya Jamii Ndugu Oscar Mwakasege kutoka TPDC, alipokuwa akiwasilisha mada ya utatuzi wa migogoro ya wananchi katika mradi huo.
Akiongea kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Mtaa wa Masasi ya leo Bwana Saidi Ismail Lihoka alisema, “Tunaipongeza Serikali na Shirika la TPDC kwa kutimiza ahadi yao ya kulipa fidia wananchi watakaopisha mradi wa LNG.
Pia, nitumie fursa hii kuwaasa wananchi wenzangu kwamba, wawe watulivu na wafuate utaratibu uliopangwa na TPDC katika kufanikisha zoezi hili.” Mhandisi wa Petroli Kutoka TPDC Ndugu Felix Nanguka akitoa mada ya masuala ya fidia kwa waathirika wa mradi wa LNG katika Mtaa wa Likong’o, Manispaa ya Lindi Mnamo Desemba, 2015 Serikali ilitwaa ardhi ya iliyokuwa shamba la mkonge na kuipatia TPDC hati ya umiliki wa eneo hilo kwa ajili ya kuendeleza mradi wa LNG.
Aidha, uthamini wa ardhi ya mradi ulifanyika mwaka 2015 na kufanyiwa marekebisho madogo mwezi Aprili 2017, ili kufidia eneo la ardhi ambalo lilikuwa linamilikiwa na wananchi pamoja na maendelezo yaliyofanywa na wananchi katika eneo ambalo limetwaaliwa na Serikali.
Mradi huu ni mkubwa na wa aina yake kwa Tanzania, ambao Serikali inajipanga vyema ili kuhakikisha maslahi mapana yanapatikana kwa Watanzania.
Lengo la mradi huu ni kuiwezesha Tanzania kuzalisha gesi nyingi iliyogundulika baharini na kuuza rasilimali hii katika soko la Dunia, pamoja na kuwezesha upatikanaji wa gesi ya kutosha katika soko la ndani kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme na matumizi mbalimbali ya viwandani na majumbani.
0 comments:
Post a Comment