Sunday, 10 May 2020

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAENDELEA KUHAMASISHA WAZALISHAJI KUTENGENEZA VIFAA KINGA DHIDI YA COVID - 19

...

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akizungumza katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Consumer's Choice limited Bi.Frida Mlingi (katikati) katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Consumer's Choice limited Bi.Frida Mlingi akieleza namna walivyotumia ethanol kutengeneza product mbalimbali ikiwemo mafuta kwaajili ya jiko la kisasa la kupikia.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (Kushoto)akikabidhi ethanol kwa wizara ya afya katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (Kulia)akikabidhi ethanol Shirika la Viwanda Vidogo SIDO katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (Kushoto)akikabidhi ethanol kwa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO) katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akishuhudia shughuli ya utengenezaji vitaka mikono ukiendelea katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akinawa mikono kwenye maji tiririka na sabuni katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.

********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Shirika la Viwanda Vidogo SIDO pamoja na Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO) wametakiwa kutumia malighafi (ethanol) vizuri kuokoa maisha ya watanzania kwa kuzalisha vitakasa mikono vyenye bei nafuu.

Ameyasema hayo leo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya katika hafla ya kukabidhi malighafi (Ethanol) kwa ajili ya kutengenezea vitakasa mikono katika kiwanda cha Consumer's Choice Jijini Dar es Salaam.

Aidha Mhe.Stella ametoa wito kwa wenye viwanda vya kutengeneza vifaa kinga nchini kuongeza bidii katika uzalishaji ili kuwezesha maeneo yote ya nchi kupata vifaa hivyo kwa urahisi na kwa bei nafuu.

"Nimefarijika kuona kuwa kiwanda cha Consumer’s Choice pamoja na kuchangia usafirishaji wa mali ghafi hii pia mmejikita katika kutengeneza vitakasa mikono, nawasihi wadau wengine wenye viwanda vyenye mifumo inayoweza kutengeneza vitakasa mikono tuweke nguvu kwenye uzalishaji wa vifaa hivi kwa wingi ili kusaidia mapambano haya". Amesema Mhe.Stella.

Nae Mkurugenzi wa biashara Kilombero Sugar Company Limited Bw.Fimbo Butallah amesema kuwa wao kama kampuni wamekuwa na kiwanda pia cha kutengeneza ethanol hivyo wameona nao washirikiane na serikali katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona wametoa lita 30,000 za ethanol bure kwa serikali ili iweze kuzalisha vitakasa mikono na kuvigawa kwa watanzania kwa urahisi na kwa bei iliyo na nafuu.

"Wenzetu wa Consumer's Choice kwasababu wapo kwenye viwanda wao waliomba kuisaidia serikali wakaisomba ethanol yote kutoka kiwandani mpaka hapa Dar es Salaam lakini pia wakaenda hatua moja zaidi wakaanza kuengeneza vitaksa mikono kwaajili ya serikali". Amesema Bw.Fimbo.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Consumer's Choice limited Bi.Frida Mlingi amesema kuwa kutokana na kikao kilichoitishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa na kuhudhuriwa na wazalishaji wa malighafi zinazotumika kutengenezea vitakasa mikono (hand Sanitizer), kampuni hiyo kwa kuona umuhimu kwenye mapambano ya vita dhidi ya Corona, waliahidi kusafirisha lita 30,000 za ethanol zilizotolewa na kiwanda cha Kilombero Sugar Company Limited.

Hata hivyo Bi.frida amesema kuwa pamoja na ahadi hiyo kampuni hiyo iliamua kubadili 75% ya Ethanol iliyokuwa itumike kwa kutengenezea vilevi itumike kutengenezea vitakasa mikono (hand Sanitizer) na 25% pekee ndo itumike kutengenezea vilevi, dhumuni kubwa likiwa ni kushirikiana na serikali katika mapambana dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

"Kwa kushirikiana na kampuni ya kuzalisha products za usafi (G&Co. Cleaning & Sanitation Limited) tumefanikiwa pia kutengeneza vitakasa mikono lita 11,000 zilizotokana na lita 8,000 za ethanol kati ya lita 20,000 walizopewa wizara ya afya". Amesema Bi.Frida.

Pamoja na hayo Bi.Frida amesema kuwa wapo tayari kushirikiana na serikali katika mapambano haya kwa kutoa kipaumbele kwenye vifaa kinga ili kufanikisha mapambano haya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha product za usafi (G&Co. Cleaning & Sanitation Limited Mhandisi Aswile Simon amesema kuwa wametengeneza vitakasa mikono 11,000 na kuzigawa kwa wizara ya Afya kwa kushirikiana na kampuni ya Consumer Choice na lengo lao ni kushirikiana na serikali kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mwakilishi wa Wizara ya Afya ofisi ya mganga Mkuu wa Serikali Bi.Neema Nagu amesema kuwa tokea maambukizi ya Corona kuwepo hapa nchini wizara imekuwa ikifanya kazi kila kukicha ili kuahikikisha inalinda afya za watanzania.

Vilevile Bi.Neema ameyashukuru makampuni yanayojitahidi kushirikiana na serikali kupambana dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger