Saturday, 9 May 2020

Waziri wa Ujenzi Isack Kamwelwe azindua huduma ya Tiketi Mtandao kwa ajili ya Wananchi kununua tiketi za mabasi kupitia simu zao za mkononi

...
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe amezindua majaribio ya awali ya mfumo wa ukataji tiketi za mabasi kwa njia ya mtandao nchini utakao simamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Aridhini (LATRA) .

Waziri Kamwelwe amezindua mfumo huo jijini Dar Es salaam ambapo amesema kuwa mfumo huo uliotengenezwa na Kituo cha Taifa cha Kutunza Taarifa (NIDC) utasaidia kupunguza msongamano katika vituo na kurahisisha huduma ya ukataji tiketi kwa wasafiri.

“Mfumo huu wa tiketi mtandao utatatua changamaoto za muda mrefu katika sekta ya usafiri, kwani utakuwa na taarifa zote muhimu ambazo zinaweza kutumiwa na taasisi kama Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) ambazo zinahusika na takwimu, sera na utafiti” Amesema Waziri Kamwelwe

Waziri Kamwelwe amesema kuwa mfumo huo unafaida kwa wamiliki wa mabasi na watumiaji wa usafiri, ambapo utaondoa upotevu wa mapato kwa wamiliki yaliyokuwa yanapotea kwenye mikono ya wapiga debe.

Waziri amesema mfumo huo upo tayari kutumika kwa majaribio hadi mwisho wa mwezi juni 2020 kwa usafiri wa mabasi ya masafa marefu na ifikapo septemba 2020 utekelezaji wa mfumo huo utaanza kwenye mabasi ya mjini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Gilliard Ngewe, amesema kuwa matumizi ya tiketi mtandao yataleta mabadiliko makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini kwani watoa huduma na mawakala hawataweza kuwadanganya wamiliki wa mabasi kwani taarifa zitakuwepo kwenye mfumo.

“Suala la kumfungia tajiri hesabu halitakuwepo kwani tajiri atajifungia hesabu yeye mwenyewe”Amesema Ngewe

Amesma kuwa matumizi ya tiketi mtandao yataondoa orodha ya abiria iliyokuwa inapigwa muhuri na Jeshi la Polisi kwani orodha hiyo itapatikana kwa njia ya mtandao.

Ameongeza kuwa suala la abiria kulanguliwa nauli kila ifikapo kipindi cha mwisho wa mwaka limekwihsa kwani abiria anaweza kukata tiketi kwa kutumia simu yake ya mkoni bila kufika kituo cha mabasi.

Ngewe amesema kuwa LATRA imejipanga kusimamia mfumo huo kikamilifu kwani kutakuwa na kituo maalum cha kutoa huduma kwa wateja ambapo wataweza kupiga simu na kupatiwa huduma kwa saa 24 kwa kupiga namba 0800110150.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger