Tuesday, 12 May 2020

WALIOFARIKI KWA CORONA NCHINI MAREKANI WAFIKA 81,795

...

Kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la habari la Reuters, idadi ya vifo vinavyotokana na janga la Corona imefikia zaidi ya 81,795 nchini Marekani.

Hayo yanajiri wakati hatua ya kulegeza vizuizi vya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo imeanza kutekelezwa katika majimbo mengi nchini humo.

Idadi ya vifo vinavyotokea ya kila siku imeongezeka kwa wastani hadi 2000 tangu katikati ya mwezi wa Aprili, licha ya hatua zinazotekelezwa kumaliza janga hilo.

Idadi hii iko juu zaidi ya ile ya homa ya msimu kwa miaka yote tangu mwaka 1967, pia inazidi ile ya UKIMWI kwa kipindi cha miaka ya 1981 hadi 1992, ikimaanisha miaka kumi na moja kufuatia kuanza kwa ugonjwa huo.

Kuhusu idadi ya visa vya maambukizi, zaidi ya watu milioni 1.3 wamepata virusi vya Corona na idadi ya jumla ya kila siku inaendelea kuongezeka, hasa huko Mississippi, Minnesota na Nebraska.

Kwa upande mwingine, idadi ya maambukizi imepunguka katika jimbo la New Jersey na Jimbo la New York


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger