Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu wake wa Rais Mike Pence wamelazimika kupima tena corona baada ya Mwanajeshi anayefanya kazi Ikulu kubainika ana corona, Trump na Pence wote ni wazima, hawajakutwa na virusi hivyo.
"Tuna vipimo bora kuliko Nchi zote Duniani, nimepima jana na leo pia na sina corona, kupima sio kitu kigumu, imenishangaza kuona Mtu wangu wa karibu ana corona namfahamu ni Mtu mzuri, ila ndio hivyo wasiwasi umetanda kila kona unaweza kukutana na Mtu ni mzima, kesho ukasikia tayari ana corona”- Amesema Trump
Hadi mapema leo hii vifo vitokanavyo na Virusi vya corona Nchini Marekani vimefikia 76,938 na visa 1,292,623 ikiwa ndiyo Nchi inayoongoza Duniani kwa wagonjwa na vifo.
Hispania visa 256,855 na vifo 26,070, Italia visa 215,858 na vifo 29,958, Uingereza visa 206,715 na vifo 30,615 ikiwa ndiyo Nchi inayoongoza kwa vifo vya corona kwa Bara la Ulaya.

0 comments:
Post a Comment