Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad ( CCM) amekabidhi gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto katika Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mhe. Azza Hilal Hamad amekabidhi gari hilo leo Ijumaa Mei 8,2020 kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko katika Kituo cha Afya Tinde kilichokuwa kinakabiliwa na ubovu wa gari ambalo lilikuwa linagharimu shilingi milioni 5 kila mwezi kwa ajili ya matengenezo.
Akizungumza wakati kukabidhi gari hilo,Mhe. Azza aliishukuru Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuboresha huduma za afya ili wananchi wapate huduma bora za afya.
“Mwezi Julai mwaka 2018 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika ziara yake mkoani Shinyanga alitembelea kituo cha afya Tinde akajionea hali yake. Tukiwa tunaendelea na Ziara katika Halmashauri nilimuomba atusaidie gari la wagonjwa kwa ajili ya Ushetu lakini katika kujibu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliahidi serikali italeta magari kwa ajili ya Ushetu na Tinde na leo ninakabidhi gari hili katika kituo hiki cha Tinde”,alieleza Mhe. Azza.
Mbunge huyo pia ametoa shilingi Milioni 1 kwa ajili kuchangia ujenzi wa Uzio wa Kituo cha Afya Tinde pamoja shilingi 2,500,000/= kusaidia ujenzi wa wodi ya wazazi katika Zahanati Lyabukande pamoja shilingi 2500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi zahanati ya Mwamanyuda.
Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Tinde, Dkt. Greyson Matogo alisema kituo hicho kinakabiliwa na upungufu wa watumishi wa afya na kwamba gari la wagonjwa lililopo ni bovu na mara kwa mara limekuwa likiharibika na kujikuta wakitumia shilingi milioni 5 kwa ajili ya matengenezo kila mwezi.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko alimshukuru Mbunge Azza Hilal kwa namna anavyotolea kusaidia wananchi ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi.
Kuhusu changamoto ya upungufu wa watumishi wa afya, Mkuu huyo wa wilaya alisema serikali italeta watumishi wawili katika kituo cha afya Tinde, Samuye wawili na Kambarage mmoja.
Mboneko aliwataka wananchi kuendelea kuchangia miradi ya maendeleo ikiwemo kuchangia uzio wa kituo cha afya Tinde huku akiwahakikishia kuwa serikali itaendelea kuboresha huduma za afya kwani Rais Magufuli anapenda kuona wananchi wanapata huduma bora za afya.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Gari la kubebea Wagonjwa ‘Ambulance’ lililokabidhiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad ( CCM) kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufanya ziara katika kituo cha Tinde Mwaka 2018. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad ( CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na Serikali katika Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kadi ya gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko funguo ya gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akionesha funguo ya gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa ndani ya gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiendesha gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akishuka ndani ya gari la kubebea Wagonjwa ‘ Ambulance’ lililotolewa na serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza baada ya kukabidhiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad gari la wagonjwa kwa ajili ya kituo cha afya Tinde.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba funguo za gari la wagonjwa katika kituo cha afya Tinde.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akikabidhi kadi ya gari la wagonjwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba na Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Nicodemus Simon.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba akikabidhi kadi kwa Mganga Mfawidhi kituo cha afya Tinde Dkt. Dkt. Greyson Matogo na Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Shinyanga Dkt. Fidelis Mushi.
Viongozi mbalimbali wa serikali na CCM wakipiga picha ya pamoja.
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad ( CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko shilingi 1,000,000/= alizotoa kuchangia ujenzi wa uzio katika kituo cha Afya Tinde pamoja na shilingi 100,000/= iliyotolewa na Paroko wa Parokia ya Usanda, Padri Josephat Mahalu kusaidia ujenzi wa uzio huo. Mhe. Azza pia amechangia shilingi 2,500,000/= kusaidia ujenzi wa wodi ya wazazi katika Zahanati Lyabukande shilingi 2500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi zahanati ya Mwamanyuda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba shilingi Milioni 1.1 zilizotolewa na Mbunge Azza Hilal na Paroko wa Parokia ya Usanda, Padri Josephat Mahalu kusaidia ujenzi wa uzio wa kituo cha afya Tinde.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad ( CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko shilingi 1,000,000/= alizotoa kuchangia ujenzi wa uzio katika kituo cha Afya Tinde pamoja na shilingi 100,000/= iliyotolewa na Paroko wa Parokia ya Usanda, Padri Josephat Mahalu kusaidia ujenzi wa uzio huo. Mhe. Azza pia amechangia shilingi 2,500,000/= kusaidia ujenzi wa wodi ya wazazi katika Zahanati Lyabukande shilingi 2500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi zahanati ya Mwamanyuda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba shilingi Milioni 1.1 zilizotolewa na Mbunge Azza Hilal na Paroko wa Parokia ya Usanda, Padri Josephat Mahalu kusaidia ujenzi wa uzio wa kituo cha afya Tinde.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
0 comments:
Post a Comment