Friday, 15 May 2020

MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA YATOA MAAMUZI HATMA YA DHAMANA YA MBUNGE SULEIMAN NCHAMBI

...
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 15,2020 imetoa maamuzi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoa wa Shinyanga Suleiman Nchambi (CCM) anayeshtakiwa kwa makosa 12 ya Uhujumu Uchumi ana haki ya kupewa dhamana kwa masharti.

Akitoa maamuzi ya maombi ya dhamana hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Phocus Mkeha, ambaye alikuwa akisikiliza maombi ya dhamana hiyo amesema Mbunge huyo ana haki ya kupewa dhamana kwa masharti ya kusaini bondi ya Shilingi Milioni 50, na mdhamini wake bondi ya Milioni 10, pamoja na kushikiliwa Hati yake ya kusafiria 'Passport'.

Aidha amesema maamuzi ya utoaji wa dhamana hiyo ameyarudisha katika mahakama ya wilaya ya Shinyanga mahali kesi yake ya msingi ilipoanzia ambapo wao ndiyo watasimamia masharti ya utoaji wa dhamana hiyo.





Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger