Ofisi ya TAKUKURU Kiteto, imemfikisha mahakamani katibu wa baraza la ardhi kata ya Sunya, Hamisi Hemedi Saidi kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) pamoja na kifngu cha 15 (2) vya sharia ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007.
Akisomewa mashitaka mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya ya Kiteto, Joakim Mwakiyolo, mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Wilayani humo, Wakili Yahaya Masakilija alisema, mtuhumiwa ni mkazi wa Kijiji cha Sunya na katibu wa Baraza la Ardhi katika kata hiyo, tarehe 4.5.2020 aliomba rushwa ya shilingi 200,000 kutoka kwa mwananchi ili ampe tahafifu ya kesi yake ambayo imesajiliwa kwake namba 13/2019.
Shitaka la pili tarehe 5.5 2020 mtuhumiwa huyo tena akiwa katika nafasi yake ya ukatibu wa baraza, aliomba na kupokea rushwa ya kiasi cha shilingi laki 120,000 kama kishawishi ili aweze kumsaidia kushinda kesi shauri la ardhi namba 13/2019 ambalo lipo katika baraza lake hilo.
Katika mashitaka hayo yote mawili mshitakiwa Hamisi Hemedi Saidi alikana shitaka na yupo nje kwa dhamana, kesi hiyo ya Jinai namba 55/2020 itaendelea kusikilizwa hoja za awali mahakama ya wilaya ya Kiteto tarehe 9.6.2020.
0 comments:
Post a Comment