Sunday, 10 May 2020

Iran Yasema Iko Tayari Kubadilishana Wafungwa na Marekani

...
Msemaji wa serikali ya Iran Ali Rabiei amesema kuwa Marekani bado haijajibu ombi lao la kubadilishana wafungwa.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kishwahili DW, Rabiei amesisitiza kuwa Tehran iko tayari kubadilishana wafungwa na Marekani bila masharti yoyote.

Iwapo hilo litatokea, basi itakuwa ni mojawapo ya matukio machache ya ushirikiano kati ya Marekani na Iran, mataifa mawili ambayo yamekuwa kama mfano wa pamba na moto.

Uhusiano wa Marekani na Iran umezidi kuwa mbaya hasa baada ya Rais Donald Trump kuingia madarakani

Kumetolewa wito na nchi zote mbili kubadilishana wafungwa kutokana na janga la virusi vya Corona.

Katika eneo la Mashariki ya kati, Iran imeathirika pakubwa na janga hilo nayo Marekani ikiongoza kwa idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Covid 19 kote duniani.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger