Wednesday, 13 May 2020

Halmashauri Ya Wilaya Misenyi Yakusanya Zaidi Ya Bilioni 2 Mapato Yandani Kwa Mwaka Wa Fedha 2019/2020

...
Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Halmashauri ya wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera imefanikiwa kwa kiwango kikubwa cha  ukusanyaji wa mapato ya ndani wilayani humo kutoka  bilioni 1.2 kwa mwaka wa fedha 2015/16 hadi bilioni 2.5 kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.
 
Ayo yameelezwa Mei 11 na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo (diwani wa kata ya Kyaka) Mh Projestus Tegamaisho wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa mwandishi wa mpekuzi blog mkoani kagera.
 
Akizungumza mh.Tegamaisho amefafanua kuwa kutokana na mafanikio hayo wameweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo  ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu katika sekita ya kilimo ikiwa nikuwapatia elimu juu ya uzalishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo na biashara kama miwa, ndizi, vanira na mazao mengine.
 
“Katika wilaya yetu ya misenyi  kuna uzalishaji wa mazao mbalimbali kama Ndizi, Maharage, Viazi lishe kilimo cha mahindi lakini sasa hivi tumepata zao mbadala watu wanalima Mpunga, Vanira lakini tuna kilimo cha Miwa ambalo ni zao la biashara Misenyi pamoja na kilimo cha Kahawa ”Amesema Tegamaisho
 
Miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo imetekelezwa ikiwa ni pamoja na ukarabati wa barabara zilizopo chini ya wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarura.
 
Kwa upande wa afya amesema vituo mbalimbali vya afya na zahanati zilizopo wilayani humo zimekarabatiwa nahalmashauri hiyo  tayari wamejenga zahanati mpya ya Ngando  katika kata Nsunga na kituo kipya cha afya Kabyaile kata Ishozi.
 
Aidha Tegamaisho ameeleza kuwa Zaidi  ya hekari 50 za aridhi zimetengwa na halmashauri hiyo  kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya hiyo itakayo jengwa katika kijiji Bulembo kata ya Mushasha.
 
Kuhusu sekta ya elimu amesema wakati wakiingia madarakani elimu ya msingi ufaulu ulikuwa 75.5%  lakini hadi sasa ufahulu wilayani humo  ni 84.8% na wanfunzi wote walio fahulu wamefanikiwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na wananchi wa Wilaya ya Missenyi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miundombinu ya elimu kama ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Sanjali na hayo mh Tegamaisho amesema kuwa mpaka sasa takiribani vijiji 68 kati ya vijiji 72 vya wilaya hiyo tayari vina nishati ya umeme na bado vijiji vya Bugango, Kakunyu,  Buchurago na kijiji Katano ambavyo vinatarajiwa kupatiwa umeme katika awamu itakayofuata.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger