Sunday, 10 May 2020

Barabaraya Uyogo – Ulowa Katika Halmashauri Ya Ushetu Yapandishwa Hadhi

...
SALVATORY NTANDU
Serikaili imesema kuwa barabara ya kutoka Uyogo hadi Ulowa katika halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani  Shinyanga imepandishwa hadhi na kutoka kuwa chini ya wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) nakuwa chini ya wakala wa barabara Tanzania, (Tanroads). 

Barabara nyingine ni ile inatoka Masumbwe wilayani mbogwe mkoani geita kwenda Ulankulu mkoani Tabora ambayo nayo ilikuwa chini ya Tarura Sasa itakuwa ni ya Tanroads.

Hayo yalielezwa jana  na waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Elias Kwandikwa katika kijiji cha Mbika  kata ya Ushetu,  wakati akikabidhi gari la wagonjwa katika kituo cha afya mbika,lilotolewa na serikali.
 
Alisema kuwa tayari timu ya wataalam imekwisha fanya uhakiki ili kuruhusu taratibu za kuzipandisha barabara hizo na kwamba lengo ni kutambua mchango mkubwa unaotokana na barabara hizo inazotumika kupitisha mazao ikiwamo zao la tumbaku na Pamba.

Akizungumzia msaada wa gari la wagonjwa, Kwandikwa alisema  gari Hilo lenye  thamani  ya shilingi  Milioni 120 ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri mkuu aliyoitoa wakati wa ziara yake katika halmashauri ya Ushetu.

Aidha Kwandikwa alisema kuwa lipo gari lingine la wagonjwa  ambalo ni aina ya naoh ambalo litaletwa hivi karibuni kwaajilibya kusaidiabkubeba wagonjwa.

Akipokea msaada wa gari Hilo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Ushetu Michael Matomora alisema gari Hilo litatumika katika kituo Cha afya Mbika kutokana na kituo hicho kuwa kinahudumia  wagonjwa wengi kutoka halmashuri hiyo na  kata jirani za mkoa wa Tabora, na kwamba gari Hilo pia litasaidia vituo vya afya jirani katika  halmashauri ya UShetu.

Naye Diwani wa kata ya Ushetu Pili Sonje aliipongeza serikali kwa msaada huo na kwamba Sasa itarahisisha kwa Kiasi kikubwa kuhudumia wagonjwa hasa kina mama wanaopatabrufaa ya kwenda katika hospitali ya halmashuri ya mji wa Kahama na wanaopewa rufaa ya kwenda Shinyanga au Bugando.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha alitoa wito kwa watumishi na wananchi kwa ujumla kuwa na desturi ya kutunza rasilimali za umma ili ,ziweze kudumu na kunisaidia jamiii huku Aliwakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhali ya ugonjwa wa Covid 19 unaosabaishwa na virusi vya Corona.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger