Jamaa mmoja mwenye miaka 65, kutoka kijiji cha Sikuvale, eneo bunge la Navakholo, Kakamega nchini Kenya amekamatwa kwa madai ya kumchapa hadi kumuua mke wake mwenye miaka 56.
Elphas Munyanda, anadaiwa kurejea nyumbani usiku wa Jumatatu, Mei 11, akiwa mlevi chakari na kuanza kumchapa mke wake Elizabeth Naswa.
Munyanda alikuwa anadai kwamba marehemu alimpokonya simu yake kwa sababu alikuwa anashuku kwamba ana mahusiano ya kando na mwanamke mwingine.
Kulingana na ripoti ya K24, majirani ya wawili hao walishuhudia kwamba wamekuwa na ugomvi wa kila mara huku madai ya kutokuwa na uaminifu katika ndoa ukiwa chanzo cha vita vyao vya kila mara.
Mzee wa kijiji hicho Boniface Monde Namwacha, aliwaambia wanahabari kuwa marehemu aliaga dunia papo hapo baada ya kuelemewa na majeraha.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kakamega na mshukiwa kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Navakholo.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kakamega na mshukiwa kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Navakholo.
Polisi bado wanafanya uchunguzi kuhusiana na suala hilo.
0 comments:
Post a Comment