Sunday, 5 April 2020

Wagonjwa wawili wa corona waongezeka Zanzibar, Sasa Wamefika 7

...
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza uwepo wa wagonjwa wawili wapya wenye maambukizi ya virusi vya corona visiwani humo na sasa jumla wamefikia saba.

Taarifa ya Waziri Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed imeeleza kuwa wagonjwa hao ni raia wa Tanzania ambao kwa nyakati tofauti waliingia visiwani Zanzibar kutokea mkoani Tanga.

Mohamed amesema watu hao waliingia kupitia bandari ya Mkokotoni mmoja ni mwanaume mwalimu wa shule wa mkoani Tanga aliingia Machi 18 na mwingine ni mfanyakazi wa hoteli (27) alienda Tanga Februari na kurudi Machi 13.

“Wagonjwa wote wanaendelea na matibabu katika kituo cha matibabu ya corona cha Kidimni na hali zao zinaendelea vizuri” imeeleza taarifa ya Mohamed


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger