Monday, 13 April 2020

Tanzia : MWANAHARAKATI WA HAKI ZA WATU WENYE UALBINO JOSEPHAT TORNER AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

...

Josephat Torner enzi za uhai wake

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na Utetezi wa haki za Watu wenye Ualbino iitwayo Foundation of Josephat Torner Europe Aid (FOJOTEA) ambaye amewahi kuwaAfisa Mahusiano na Habari wa Chama cha watu wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner (40) amefariki dunia baada ya kugongwa na Hiace ‘ Daladala’ akivuka barabara jijini Mwanza.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema Josephat Torner amefariki dunia jana Aprili 12,2020 majira ya saa mbili usiku baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T263 CZQ Toyota Hiace Daladala. 

“Josephat Torner mkazi wa Gana Mwanza ambye ni mtu mwenye ualbino aligongwa na Daladala na kufariki dunia katika barabara ya Makongoro eneo la Kifua wazi karibu na Rock City Mall kata ya Kirumba iliyoendeshwa Emmanuel Mwanasalaha”,amesema Kamanda Muliro. 

“Daladala hiyo iliyokuwa inatokea Mjini kwenda Nyakato ilimgonga Josephat Torner ambaye alikuwa akivuka barabra kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine",amesema Kamanda

Kamanda Muliro amesema dereva wa gari hiyo alikimbia na kutelekeza gari na Jeshi la polisi linamshikilia mmiliki wa gari hiyo huku juhudi za kumtafuta dereva wa gari zikiendelea.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger