Friday, 17 April 2020

NFRA Kuanza Kununua Mahindi, Mtama Na Mpunga-milton Lupa

...
Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeanza kujipanga kuanza kununua mazao ya nafaka kwa wakulima ili punde tu mazao yatakapovunwa shambani yaweze kununuliwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya akiba ya chakula.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Milos Lupa amemuhakikishia katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Kilimo Ndg Jerald Kusaya wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja NFRA Makao makuu Jijini Dodoma kuwa tayari wataalamu wapo mikoani kwa ajili ya kazi hiyo.

Lupa amesema kuwa msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 NFRA itanunua mazao makuu matatu ambayo ni zao kuu la chakula Mahindi, Mpunga na Mtama.

Amesema kuwa lengo la serikali kuamua kununua mazao hayo matatu ni kujiimarisha vyema katika uhifadhi wa chakula ili inapotokea dharula ya chakula nchini kuwe na hifadhi ya mazao tofauti tofauti.

Akizungumzia lengo la Wakala kuanza kujipanga ili kununua nafaka mapema, amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kupata mazao bora kwa ajili ya kuhifadhi kadhalika kupata mazao mengi.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger