Wednesday, 15 April 2020

Dar es Salaam yatenga vituo 25 vya kukusanya sampuli za vipimo vya Corona....Tazama Hapa

...
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda ametanagza vituo 25 katika jiji la Dar vitakavyotumika kukusanya sampuli za vipimo vya ugonjwa wa Covid-19 kwa wagonjwa watakaohisiwa kuwa na maambukizi. 


Vituo hivyo ni pamoja na hospitali za rufaa za mikoa, vituo vya afya na hospitali binafsi.

Taarifa hiyo imesema kuwa manispaa ya Kinondoni itatumia vituo sita vikiwemo hospitali za Mwananyamala, Magomeni, Mikoroshini, IST, TMJ na Rabininsia.

Manispaa ya Ilala vituo vitakavyotumika ni Amana, Buguruni, Mnazi mmoja, Muhimbili, Hindu Mandal, Aga Khan na Regency.

Vituo vingine vilivyoteuliwa katika manispaa ya Temeke ni hospitali ya Temeke, Mbagala Rangi Tatu, Yombo na TOHS.

Vituo vitakavyotoa huduma hiyo katika manispaa ya Ubungo ni pamoja na Sinza, Kimara, Mloganzila na Bochi na manispaa ya Kigamboni vitatumika vituo vitatu vya  Vijibweni, Kigamboni na Agha Khan.

==>>Msikilize hapo chini


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger