Saturday, 4 April 2020

Breaking : GARI YAUA WATU WANNE BAADA YA KUGONGA GEMA NA KUTUMBUKIA BWAWANI BARABARA YA OLD SHINYANGA

...


Gari yenye namba za usajili T.785 DBM Toyota IST ikitolewa bwawani na Trekta baada ya kugonga gema na kutumbukia katika bwawa hilo na kuua watu wanne  katika eneo la kitongoji cha Mwajinaganya kijiji cha Bubiki B, kata ya Bubiki, tarafa ya Mondo, wilaya ya Kishapu barabara ya Old Shinyanga kuelekea Bubiki - Mwanza . Picha zote na Malunde 1 blog

Sehemu ya bwawa hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba  akiwa katika eneo la kitongoji cha Mwajinaganya kijiji cha Bubiki B, kata ya Bubiki, tarafa ya Mondo, wilaya ya Kishapu barabara ya Old Shinyanga kuelekea Bubiki - Mwanza ambapo gari yenye namba za usajili T.785 DBM Toyota IST imegonga gema na kutumbukia bwawani.
Gari yenye namba za usajili T.785 DBM Toyota IST iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye Gration Mlikozi iliyopoteza uelekeo na kugonga gema na kutumbukia katika bwawa la maji lilipo pembezoni mwa barabara ya vumbi ya Old Shinyanga na kuua watu wanne.


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 
Watu wanne wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wanasafiria kugonga gema kisha kutumbukia katika bwawa lililopo pembezoni mwa barabara ya vumbi ya kutoka Old Shinyanga kuelekea Bubiki hadi Mwanza kwenye kijiji cha Bubiki B kata ya Bubiki wilaya ya Kishapu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema ajali hiyo ya gari kuacha njia na kugonga gema na kutumbukia katika bwawa la maji na kusababisha vifo imetokea leo Jumamosi Aprili 4,2020 majira ya saa saa tatu na dakika 20 katika eneo la kitongoji cha Mwajinaganya kijiji cha Bubiki B, kata ya Bubiki, tarafa ya Mondo, wilaya ya Kishapu. 

“Ajali hii imetokea katika barabara ya vumbi ya kutoka Old Shinyanga kuelekea Bubiki hadi Mwanza ambapo ,gari yenye namba za usajili T.785 DBM Toyota IST iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye Gration Mlikozi, miaka haifahamiki, ilipoteza uelekeo na kugonga gema na kutumbukia katika bwawa la maji lililochimbwa kwa ajili ya kuchukulia udongo wa matengenezo ya barabara na kusababisha vifo kwa watu wanne”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

Amewataja waliofariki dunia katika ajali hiyo ni dereva wa gari hilo Gration Mlikozi pamoja na abiria watatu ambao ni Singu Isack Lazaro (57), Chrispin Ikate, miaka haijulikani, mwanaume, na Abdallah Mussa, mwanaume, miaka haifahamiki. 

“Chanzo cha ajali ni mwendokasi wa gari husika katika barabara ya vumbi kulikopelekea dereva gari kumshinda na kwenda kugonga gema na kutumbukia katika bwawa la maji na kusababisha vifo”,amesema. 


“Gari husika limeshatolewa katika maji na lipo katika kituo cha polisi Maganzo. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga. Natoa wito kwa madereva wote kutii sheria za usalama barabara na kuacha kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi”,amesema Kamanda Magiligimba.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger