Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Wizara ya Maji imetoa tahadhari kwa wananchi wote wakiwemo wamiliki wa mabwawa ya maji na mabwawa ya tope sumu kuzingatia matangazo ya utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kuhusu mvua za masika za mwaka huu kuwa ni juu ya wastani katika maeneo mengi nchini.
Katika taarifa iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano ,Serikalini kupitia Wizara ya Maji imefafanua kuwa mvua hizo zinaweza kusababisha mabwawa kujaa maji zaidi ya uwezo wake hivyo kutishia usalama wa wananchi,mali zao na mazingira kwa ujumla.
Taarifa hiyo imesema kuwa mabwawa yanaweza kupasuka kwa sababu ya kujaa au kutiririsha maji katika mikondo isiyo rasmi [overflow]na miongoni mwa madhara yake ni kuleta mafuriko katika vijiji,barabara,madaraja na kuharibu miundombinu mingine.
Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa mwaka huu kuwa na mvua nyingi katika maeneo mbalimbali nchini Wizara imewataka wamiliki wote wa Mabwawa kutekeleza mambo matatu ambayo ni kusafisha utoro wa maji,kudhibiti maji yasisambae katika mazingira pamoja na kuwasilisha mipango ya usalama wa mabwawa na mafuriko kwa mkurugenzi wa Rasilimali za maji ili kukabili dharura itakayotokea kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha kama sheria ya Rasilimali za Maji Na.11 ya mwaka 2009 sehemu ya kumi[x] na kanuni zake za Usalama wa Mabwawa GN .237 za Mwaka 2013 kifungu cha 16 inavyoelekeza.

0 comments:
Post a Comment