Friday, 6 March 2020

WAFANYABIASHARA MBOGWE WAKERWA MAJITAKA SOKONI

...
Na Salvatory  Ntandu - Mbogwe
Wafanyabiashara katika soko kuu la Halmashauri ya Mbogwe Mkoani Geita, wamesema wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kusambaa kwa maji taka yanayotoka katika choo cha soko hilo na kuomba Idara ya afya ya halmashauri hiyo kuchukua hatua za haraka kukabiliana na suala hilo.

Charles Issa ni mmoja wa wafanyabiashara aliyetoa malalamiko hayo mbele ya kamati ya siasa ya wilaya ya Mbogwe ya Chama cha mapinduzi (CCM), iliyofika katika soko hilo kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha mwaka mwaka 2015 kuanzia mwezi Julai hadi Desemba 2019.

Alisema kuwa, maji hayo yasipoondolewa kwa haraka katika eneo hilo yanaweza kuhatarisha afya za wa wateja wao wanaofika katika soko hilo ili kupata mahitaji yao mbalimbali na kuomba kero hiyo ipatiwe ufumbuzi wa haraka kabla haijaleta madhara kwa wakazi wa eneo hilo.

“Sisi wafanyabiashara wa soko hili tozo mbalimbali ikiwemo za choo na usafi kila mwezi lakini usafi wa soko choo hiki umekuea kero kutokana na kujaa maji taka huku halmashauri yetu ikiwa haijachukua hatua zozote”,alisema Issa.

Naomi Kashindye ni mmoja wa wafanyabiashara wa soko hilo alisema kuwa,kila wiki wanatozwa kiasi cha shilingi 1,000 kwa ajili ya usafi wa soko hilo,lakini cha kushangaza soko ni chafu na bado choo kimejaa na kuririsha majitaka ambayo ni hatari kwa afya hasa Mama ntilie waliko jirani na choo hicho.

Akijibu malalamiko ya wafanyabiasha hao kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe, Peter Lumuva alisema, kuwa watahakikisha waitatua kero hiyo kwa haraka ikiwa ni pamoja na kuyaondoa maji hayo ili yasiweze kuleta madhara kwa wananchi wanaoishi katika eneo.

“Nitakaa na viongozi wa soko hili ili kuangalia namna bora ya kuliendesha pamoja kuiagiza idara yetu ya afya kuja kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa mama ntilie ili wasiendelee kumwaga maji na kutupa takataka ovyo katika eneo la soka”,alisema Lumuva.

Akizungumza na Kaimu Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbogwe ambaye pia ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbogwe Gress Shindika, alitoa wiki moja kwa mzabuni na uongozi wa soko hilo kuhakikisha wanaondoa majitaka katika eneo hilo sambamaba na taka ngumu zilizopo katika soko hilo.

“Maafisa afya wa Halmashauri ya Mbogwe tembeleeni soko hili kwa mara ili kutatua changamoto na kuzitatua zinazowakabili wafanyabiashara katika soko hilo,na kuacha kwenda kwenye maeneo ya migodi midogo”alisema Sindika.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger