Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) nchini Tanzania kimewataka wanafunzi wote kuhakikisha ifikapo Ijumaa Machi 20, 2020 wawe wameondoka kurejea nyumbani.
UDSM imetoa taarifa hiyo Jumatano Machi 18,2020 baada ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kutangaza kuvifunga vyuo vyote kutokana na kujikinga na virusi vya ugonjwa wa corona (CODIV-19).
Katika taarifa ya Makamu mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye imesema katika kutekeleza maelekezo na ushauri wa Serikali kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo, shughuli zote za masomo chuoni hapo zimesitishwa kuanzia leo Machi 20 2020 hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.
0 comments:
Post a Comment