Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitishwa kwa safari za ndege kutoka nchini humo hadi barani Ulaya kama mbinu ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Trump amesema, marufuku hayo yatatekelezwa kwa muda wa siku 30 zijazo kuazia siku ya Ijumaa lakini hatua hii haitaithiri Ireland na Uingereza, ambayo ina maambukizi 460.
"Ili kuzuia visa vipya maambukizi ya Covid-19 kuingia katika nchi yetu, nitazuia safari zote kutoka Ulaya hadi Marekani kwa siku 30 zijazo," amesema rais Donlad Trump katika hotuba yake kwa njia ya Televisheni siku ya Jumatano.
Donald Tump amenyooshea kidole cha lawama Umoja wa Ulaya akisema ''umeshindwa kuchukua hatua za tahadhari kama hizo'' zilizoanzishwa na Marekani.
Hata hivyo rais wa Marekani ametangaza kutoa mkopo wa mabilioni ya dola kwa wafanyabiashara wadogo, na kutaka bunge la Congress kupitisha nafuu ya kodi ili kukabiliana na athari za mlipuko wa corona kiuchumi.
Marekani ina maambukizi 1135 na tayari watu 38 wamepoteza maisha.
-RFI
-RFI
0 comments:
Post a Comment