Thursday, 12 March 2020

Serikali Kuanzisha Mfuko Maalum Wa Kilimo

...
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema wizara ya kilimo inakusudia kuanzisha mfuko maalum kwa ajili kusimamia maendeleo ya mazao ya pamba,tumbaku na korosho.

Ametoa kauli hiyo jana mjini Chato alipokuwa akizunguzma kwenye kongamano la kilimo kwa vijana wa mikoa ya Geita,Shinyanga na Kagera na kuutaja mfuko huo utakaojulikana kama “Seed Fund For AAgriculture”

Bashe amewaeleza vijana hao kuwa mfuko huo utakaochangiwa na wakulima ili kuondoa chanagamaoto za upatikanaji pembejeo,viuatilifu na masoko nchini

Amesema wizara inatarajia wakulima wa pamba wachangie sh .20 kwa kilo,korosho sh.20 na tumbaku sh.200 kwa kilo hivyo kuwezesha serikali kupata fedha za kutosha kusimamia changamoto za mazao haya ya kimkakati.

“Ukichukua takwimu za uzalishaji za msimu uliopita 2019 tunatarajia kukushanya fedha shilingi Bilioni 24 ambazo tutzaifungulia akaunti maalum Benki Kuu wa Tanzania kutunza fedha hizo,alisema Bashe

Aliongeza kusema taasisi za fedha kama mabenki yatapewa fursa ya kwenda kukopa kawa riba itakayokubaliwa na serikali ili waweze kudhamaini wakulima kupitia AMCOS au Ushirika kwa ajili ya pembejeo na mahitaji mengine ya shambani.

Ili kufanikisha hilo Bashe amesema kila mkulima nchini atasajiliwa na kuwa na kitabu chake kitakachoonyesha mahitaji ya shamba,kiasi cha eneo alilozalisha na mavuno yake na kiasi atakachopeshwa.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo wa Kilimo amezipongeza Benki za NMB,CRDB na Azania kwa kuwashiriki katika kukwamua ununuzi wa zao la pamba msimu wa 2019 kwa kudhamini mikopo ya wanaunuzi wa pamba kwa asilimi 13 jambo ambalo lililotoa manufaa kwa wakulima


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger