Thursday, 5 March 2020

Mkutano wa James Mbatia Wazuiwa na Jeshi la Polisi Ruangwa

...
Mkutano wa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa, James Mbatia umezuiliwa na kutakiwa kuripoti kituo kidogo cha polisi Ruangwa wilayani Rungwe na ametakiwa kutoendelea na chochote katika mkutano huo.
 
Taarifa iliyotolewa kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa chama hicho imeeleza kuwa Mbatia ambaye amefika katika jimbo la Busokelo majira ya saa tano asubuhi leo Alhamisi Machi 5, 2020 katika Kijiji cha Kandete alikuwa akisubiriwa na wanachama wa NCCR kwenye mkutano wa ndani.

Imeeleza kuwa, baada ya mkutano huo kuzuiwa, akiwa nje ya ukumbi wa mikutano Mbatia amesema kwa sasa hatozungumza lolote mpaka atakapofika polisi na kujua anaitiwa nini na kuna shida gani.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger