Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amelipa faini ya 70,000,000 na muda wowote leo Ijumaa Machi 13, 2020 atatoka katika gereza la Segerea.
Mbowe ni kati ya viongozi wanane wa Chadema ambao pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji Jumanne Machi 10, 2020 walihukumiwa kulipa faini ya Sh350 milioni au kwenda jela miezi mitano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili.
Yeye alihukumiwa kulipa faini ya sh. milioni 70 baada ya kutiwa hatiani katika mashtaka nane yakiwemo ya uchochezi.
Yeye alihukumiwa kulipa faini ya sh. milioni 70 baada ya kutiwa hatiani katika mashtaka nane yakiwemo ya uchochezi.
Tumekamilisha kumlipia Mhe.Freeman Mbowe na Sasa ni taratibu za kumtoa Magereza zinafanyika ili atoke mchana huu Mara taratibu zitakapokamilika .Asanteni Sana watanzania pic.twitter.com/PtbTJhfT4j— Jon Mrema (@JonMrema) March 13, 2020
0 comments:
Post a Comment