Waziri wa ardhi,nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi,amezitaka Halmashauri zote nchini kuwa na Mipango ya matumizi bora ya ardhi katika maeneo ya vijiji ili kuwapatia wananchi hatimiliki.
Akizungumza katika kikao cha baraza la ushauri la mkoa wa Manyara (RCC), Lukuvi amesema halamashauri zikiwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi itaiwezesha serikali kupata kodi ya ardhi kwa kupima viwanja na kutoa hatimiliki kwa wananchi.
Pia Waziri Lukuvi amesikitishwa na baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri hapa Nchini ambao mpaka sasa muda wao unaisha lakini hawakuweza kutowa hatimiliki hata kwa wananchi Watano jambo linaloisababishia hasara serikali kwa kukosa mapato yake.
Kwa upande mwingine Waziri Lukuvi amemteua Kamishna Msaidizi atakaye shughulika na kero zote za ardhi mkoa wa Manyara na kuwawezesha wananchi kupata hati miliki kwa wakati.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amempongza waziri Lukuvi kwa jitihada za kukabiliana na Migogoro ya ardhi na kusema kuwa Migogoro ya ardhi inaendelea kupungua ukilinganisha na miaka ya nyuma .
0 comments:
Post a Comment