Thursday, 12 March 2020

Halima Mdee Amwaga Machozi Baada ya Kutoka Gerezani...."Watanzania hamjui ni jinsi gani mlivyotuliza, hatukutegemea "

...
Mbunge Halima Mdee amemwaga machozi hadharani baada ya kutoka gereza la Segerea leo na kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha wa kuwachangia na kuwafanyaa wao kuwa nje ya gereza.

"Watanzania nyie hamjui, hamjui mlivyotusitiri mimi ni kamanda lakini napata hisia nilikua najua tulivyonyong'onyezwa watu walivyo na aibu mbaya watakuwa wamekata tamaa ila wametuchangia tunashukuru na bado pesa zinaingia mimi nalia sio kwamba naogopa hapana ila upendo wenu muliouonyesha kwetu" alisema huku akiwa analia Halima Mdee.

Wabunge Halima Mdee, Esther Matiko na Ester Bulaya wametoka gereza la Segerea leo baada ya kulipa faini ya Sh110 milioni.

==>>Tazama hapo chini
Video Credit:EATV

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger