Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema Dereva tax aliyembeba mgonjwa wa Corona amepatikana na kuchukuliwa sampuli kwa ajili ya kutumwa Dar es Salaam ili kuona kama na yeye aliambukizwa virusi hivyo hatari vya Corona.
“Tunatafuta mtandao mzima ambao mgonjwa huyo wa Corona(Isabella) alishirikiana nao
"Tumempata Dereva na sampuli yake imepelekwa Maabara, baada ya kumshusha mgonjwa alienda nyumbani akawa na Mke na Watoto , Watoto wakaenda shuleni, Dereva alipata pia wateja wengine”- Amesema Mrisho Gambo.
Msikilize hapo chini
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameendelea kutoa taarifa juu ya hatua walizochukua au kufikia hadi sasa baada ya mgonjwa mmoja wa Corona kupatikana Mkoani Arusha. pic.twitter.com/KX3o7LbGo5— MPEKUZI (@mpekuzihuru) March 17, 2020
0 comments:
Post a Comment