Na Andrew Chale, Dar es salaam
UPEPO mkali na mvua iliyoandamana na radi imesababisha nyumba zaidi ya 20 kuezuliwa mapaa huku Kaya 50 zikikosa makazi.
Tukio hilo la aina yake limetokea masaa mawili yaliyopita ambapo katika eneo la Kimara Golani kwa 'Bibi Rosta' mwandishi wa habari hizi ameshuhudia nyumba 19 zikiwa zimezuliwa paa za nyumba huku nyumba moja ikiwa imebomoka ukuta.
Katika tukio hilo nyumba mmoja iliyobomoka imeweza kujeruji mtu mmoja aliyekuwa ndani.
Mashuhuda:
"Tunashukuru mvua wakati inanyesha nyumba nyingi hazikuwa na watu ndani.
Athari ni kubwa hatuelewi tunaomba Serikali kama itaweza ije ifanye tathimini hata msaada kidogo." Alisema Saphia mkazi wa Golani.
Eneo lililoathirika kwa wingi ni eneo la kwa Bi. Rosta kwa Mama Mzungu nyumba 7 huku upande wa Bi Rosta michungwani nyumba 8 na nyumba zingine eneo la Golab Kanisani pamoja na mapaa ya shule ya Msingi Saranga.
Hali ya muda bado ni ya mvua huku radi zikipiga na upepo watu wengi wakiwa watoweka barabarani kuwahi nyumba zao.
0 comments:
Post a Comment