Friday, 6 March 2020

Bashe Atoa Onyo Kwa Wasambazaji Viatilifu vya Kuua Wadudu Zao la Pamba

...
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe amesema wamepata taarifa kuwa baadhi ya wasambazaji  waliopewa dhabuni ya kusambaza viuatilifu vya kuua wadudu kwenye zao la pamba wanaihujumu serikali.

Bashe amesema kuwa wamegundua wasambazaji hao wamekuwa wakiuzia serikali dawa hizo kupitia bodi ya pamba kwa bei kubwa kuliko wanavyowauzia watu wenye maduka ya kuuza viuatilifu hivyo.

Ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akipokea chupa 13,000 za viuatilifu vya pamba kutoka bodi ya pamba kwa ajili ya kuwapatia wakulima wa Mkoa wa Simiyu.

Bashe amesema kuwa wamegundua kuwepo kwa hujuma hizo, kwani viuatilifu hivyo vinavyouzwa kwenye maduka hayo bei yake imekuwa rahisi, kuliko vinavyouzwa na bodi ya pamba nchini.

Kutokana na hali hiyo Naibu Waziri huyo ameiagiza bodi ya pamba, kufanya operesheni kali kwenye maduka yote yanayouza dawa hizo kuangalia kama bei ya viuatilifu inayotumika inalingana na ile ambayo wanatumia bodi.

“Hatuwezi kuwa na wasambazaji wa aina hii, waliomba wenyewe tukawapa masharti, lazima wayatekeleze, hatuwezi kuendelea kumkandamiza mkulima, bodi ya pamba ifanye opereisheni kila duka kuangalia bei za uko,” amesema Bashe.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger