Saturday, 21 December 2019

China Yaionya Marekani Na Kuitaka Iache Kuingilia Masuala Yake Ya Ndani

...
Serikali ya China imeionya Marekani na kuitaka iache hatua zake za kuingilia masuala ya ndani ya Beijing.

Onyo hilo limetolewa na Rais Xi Jinping wa China katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais Donald Trump wa Marekani.

Rais wa China amesema kuwa, Marekani inapaswa kubadilisha "matamshi na mwenendo wake hasi" kuhusiana na masuala mbalimbali kama machafuko na vurugu za Hong Kong na Xinjiang.

Hata hivyo katika ujumbe wake alioandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Donald Trump wa Marekani hakuashiria ukosoaji huo wa China kwa Washington na badala yake amedai kwamba, kumepigwa hatua katika mazungumzo ya pande mbili kuhusiana na masuala mbalimbali kama biashara, uhusiano wa pande mbili, mgogoro wa Korea Kaskazini na machafuko ya Hong Kong.
 
Hii si mara ya kwanza kwa China kukosoa siasa na utendaji wa Marekani pamoja na uingiliaji wa Washington katika masuala ya ndani ya Beijing na katika nchi nyingine za dunia.

Hivi karibuni, Geng Shuang msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa China alikosoa vikali siasa za Marekani na kusema kuwa, uingiliaji wa wazi wa serikali ya Washington katika masuala ya ndani ya nchi tofauti, umeisababishia nidhamu ya kimataifa changamoto kubwa.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger