Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema alitumia muda mrefu kufikiria kukubali ombi la kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa kutokana na Jitihada, anazofanya katika kuiletea maendeleo Tanzania pamoja na mapambano dhidi ya Rushwa, ambapo amesema alitumia mwezi mmoja kukubali ombi hilo.
Rais Magufuli amesema kuwa sababu kubwa iliyomfanya kukaa kwa muda mrefu ni kile alichokisema, ni imani yake ilikuwa ikimsuta juu ya kutopenda vitu vya bure, kama alivyokuwa amefundishwa na Baba yake mzazi pindi alipOkuwa mdogo.
Rais Magufuli amesema kuwa "nilipopewa barua ya kunipa Shahada ya Udaktari nilijiuliza kwanini mimi, sijawahi kupenda vitu vya kupewa bure, nilikaa mwezi mzima sijaijibu, dhamira yangu ilikuwa inanisuta kwanini nipewe cha bure, 'Knowledge' niliyopewa na Baba ilikuwa inanisuta"
"Nilikubali kutokana na historia yangu na Mkapa, kingine kimenisukuma kukubali, hizi hazitolewi kwa mtu binafsi ni kwa niaba ya wengi, hii shahada imetolewa kutambua mafanikio yaliyopatikana kwenye miaka 4 ambayo hayajatokana kwa ajili yangu bali Watanzania." ameongeza Rais Magufuli.
Rais Magufuli leo Novemba 21, 2019 ametukunikiwa cheti chake cha Shahada ya Heshima ya Daktari wa Falsafa katika ujenzi wa Uchumi wa Viwanda na kuwekeza kwenye miundombinu pamoja na kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa, kutoka Chuo Kikuu cha UDOM.
0 comments:
Post a Comment