Na avitus benedicto kyaruzi,Kagera
Mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Marco Elisha Gaguti amemuagiza Kamanda wa polisi mkoani humo Revocatus Malimi kuwakamata na kuwaweka ndani mara moja mkandarasi wa manispaa ya Bukoba, Mkandarasi wa Kampuni ya Mzinga Holding Company ambaye pia ni msimamizi wa ukarabati wa Shule ya Sekondari Kahororo, mkuu wa shule ya Sekondari Kahororo pamoja na kaimu mkuu wa shule ya Bukoba secondari kutokana na kushindwa kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya shule hizo kwa wakati uliopangwa.
Hayo yamejili Novemba 22,2019 baada ya Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na kamati ya Manispaa ya Bukoba Mkoani humo ilipofanya ziara mbalimbali ili kukagua baadhi ya miradi kwa upande wa manispaa ya Bukoba ikiwemo elimu, afya,pamoja na miundombinu ya barabara.
Waliokamatwa ni Mhandisi wa manispaa ya Bukoba bw,George Geofrey, Mkandarasi wa Kampuni ya Mzinga Holding Company ambaye pia ni msimamizi wa ukarabati wa Shule ya Sekondari Kahororo,bw Festo Talimo ,Mkuu wa Shule ya sekondari kahororo bw Omary Ogambage pamoja na makamu mkuu wa Shule ya Sekondari Bukoba bw,Phocus Siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wasimamizi wa miradi hiyo mkuu wa mkoa wa kagera Brigedia Gaguti amesema kuwa miradi hiyo kwa ujumla mpaka hivi sasa haifanyi vizuri na kutoa msisitizo kwa watu wanaosimamia miradi hiyo kukamilisha kwa wakati na muda uliopangwa pasipo kuomba muda wa nyongeza.
“ Watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia miradi hiyo wasimamie ili iweze kukamilika kwa muda uliopangwa lakini pale ambapo kuna uzembe tuliokuwa tukiuona katika baadhi ya maeneo tutachukua hatua sitahiki ”
Ameongeza kuwa ataendelea kuchukua hatua stahiki kwa watendaji wa miradi hiyo watakaoshindwa kukamilisha kwa wakati miradi hiyo na hakuna mkandarasi atakayeondoka mkoani Kagera kabla ya kukamilisha mradi anao simamia.
Kadhalika Brigedia Gaguti amesema kuwa miradi hiyo imepokea shilingi bilioni 12 kutoka fedha za serikali kuu kwa mwaka wa fedha kwa upande wa manispaa ya Bukoba mkoani humo na kuwataka wakandarasi kuongeza kasi ili wasije kulipa dhamana yao kwa uchungu huku akihaidi ushirikiano wa kutosha kwa wasimamizi wa miradi hiyo pale watakapo kuwa wamekwama.
0 comments:
Post a Comment