Tuesday, 19 November 2019

Mikoa 3 kutopiga kura serikali za mitaa

...
Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema mikoa mitatu haitafanya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwa wagombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepita bila kupingwa.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwita Waitara amesema jana  jijini Dar es Salaam kuwa, kati ya halmashauri za wilaya 184 nchini, 90 hazifanyi uchaguzi huo Novemba 24 mwaka huu kwa kuwa wagombea wamepita bila kupingwa.

“Katika mikoa 26 ya hapa bara, kwa taarifa ambazo tumeshapokea mpaka leo asubuhi mikoa mitatu inaonekana kwamba wagombea wa Chama Cha Mapinduzi wamepita bila kupingwa kwa hiyo kuanzia siku ya uteuzi wao ni viongozi halali na wasimamizi wameshawateua, hakuna haja ya kampeni katika eneo hilo” ameyasema hayo wakati anazungumza kwenye kipindi cha Asubuhi  kinachorushwa na kituo cha redio cha TBC Taifa cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Waitara ameitaja mikoa ambayo haitafanya uchaguzi kabisa kuwa ni Katavi, Tanga, na Ruvuma.

“Mahalali ambako mgombea alikuwa peke yake na amepita bila kupingwa kazi ya msimamizi ni kumtangaza na baada ya hapo atasubiri baada ya tarehe 24 ataapishwa na ataanza majukumu yake kwa hiyo hakuna habari ya kampeni lakini mikoa 23 itakuwa na mchakato wa uchaguzi”amesema Waitara.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo hata katika mikoa hiyo 23 uchaguzi utafanyika kwenye baadhi ya maeneo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger