Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linamshikilia bw.Erasto Matembo mwenye miaka 30 mkazi wa Kinondoni mkoani Dar Es Salaam kwa tuhuma za kujifanyaAfisa Usalama wa Taifa na kuwanyanganya wananchi mali zao.
Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Revocatus K.Malimi wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake Novemba 22/2019 na kusema kuwa mtu huyo amekamatwa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na kuongeza kuwa alikuwa akijitambulisha kwa wananchi akiwapa huduma kuwa ni Afsa Usalama wa Taifa .
Kamanda Malimi amesema kuwa mnamo Novemba 18 mwaka huu akiwa katika kijiji cha Mugoma wilayani Ngara mtuhumiwa alimkamata mtu mmoja kwa kile alichoeleza kuwa anazo taharifa za mtu huyo kumiliki siraha ya kivita isivyo halali na kwamba siraha hiyo anaitumia katika ujambazi ndipo alipompeleka katika kituo cha polisi wilayani humo.
Ameongeza kuwa mara baada ya Polisi kuanza kumhoji huyo mtu aliyekuwa amemkamata ,lakini pia kulingana na uzito wa tuhuma yake na uzito wa ofisi ya mkamataji waliamua kushiriana na mkamataji pamoja na ofisi yake ya Wilaya.
Kamanda ameongeza kuwa alifikishwa kituoni na kujitambulisha kuwa ni Afsa Usalama wa Taifa mnamo Nonemba 19 mwaka huu na walipomfanyia mahojiano alikiri kwa kinywa chake kuwa si mtumishi wa serikali bali amekuwa akitumia kama mbinu ya kujunufaisha .
Ameongeza kuwa alisalimisha siraha mbili aina ya Bastola ambazo amekuwa akizimiliki na kuzitumia katika kutaperi wananchi .
Aidha Kamanda amesema kuwa kijana huyo alihama kutoka Dae es salaam na kuja kuishi katika kijiji cha Kirusha kata ya Mgoma,Wilaya ya Ngara kwa kumfuata mke wake ambaye ni mwalimu katika shule ya msingi ya Kishura na mda wote alimwaminisha mke wake kuwa mtumishi serikalini katika idara ya usalama wa Taifa.
Kamanda Malimi ameongeza kuwa taratibu za uchunguzi zikikamilika atafikishwa mahakamani ili kujibu ntuhuma hizo pia amewaomba wananchi ambao wamewai kukutana naye na kuwafanyia kitando chochote cha dhuruma kujitokeza ili kupata ushuhuda wao.
0 comments:
Post a Comment