Monday, 19 August 2019

Watu 63 wauawa kwenye mlipuko ulitokea kwenye ukumbi wa harusi

...
Takriban watu 63 wameuawa na wengine zaidi ya 180 kujeruhiwa jana usiku baada ya kutokea mlipuko wa kujitoa muhanga kwenye ukumbi wa harusi magharibi mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Ikithitbitisha tukio hilo polisi ya Afghanistan imesema mlipuko ulitokea saa 4.40 usiku ndani ya ukumbi wa harusi wa Shahr-e-Dubai huko Kabul.

Idadi ya vifo huenda ikaongezeka kwani watu kadhaa wapo kwenye hali mahututi.

Hadi sasa hakuna mtu au kundi lolote lililotangaza kuhusika na tukio hilo.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger