

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Ocitti (wa pili kushoto) akiwa na wageni wake ,Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ,Sara Cooke (wa kwanza kulia) na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara ,Andrew Rosindell wakijiandaa kuotesha miti katika kiwanda cha Bia cha Serengeti -Moshi.




Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV
KATIKA kukabiliana na uharibufu wa Mazingira pamoja na mabadiliko ya tabia nchi Kampuni ya Bia ya Seerengeti (SBL) kwa kushirikiana na taasisi ya The Kilimanjaro Project wamezindua kampuni ya kuotesha miti 1000 kwa mkoa wa Kilimanjaro.
Zoezi la uoteshaji miti linakuja huku kukiwa na wito kutoka jumuiya ya kimaitafifa juu ya kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa kuongeza juhudi za uhifadhi wa misitu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuweka mazingira katika hali ya usalama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Akizungumza mara baada ya zoezi la kuotesha miti katika kiwanda cha SBL kilichopo Pasua katika wilaya ya Moshi ,Mkurugenzi Mtendaji wa SBL ,Mark Ocitti amesema SBL imeamua kuongeza jitihada za uhifadhi wa mazingira sit u katika maeneo yaliyo chini ya SBL bali katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
“Huu ni uthibitisho tosha kwamba SBL imejidhatiti na iko tayari kushirikiana na wadau wengine katika kutekeleza miradi yenye kuleta tija kwa jamii zetu”alisema Ocitti.
Zoezi la uoteshaji miti limehudhuriwa na ujumbe kutoka British High Commission akiwemo Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara Andrew Rosindell pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Sara Cooke waliotembea kiwanda cha Bia cha Serengeti Moshi .
Mpango wa SBL unaenda sambamba na sera ya kampuni hiyo katika kurudisha kwa jamii sehemu ya faida na umejikita zaidi katik autoaji wa huduma bora ya maji safi kupitia mradi uitwao Water of Life (WOL) .
Mpango mwingine ilionao SBL ni pamoja na kuwasaidia wanafunzi kupata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu,kuwasaidia wakulima wa ndani husuani wa vijijini pamoja na mpango wa kuhamasisha unywaji pombe kistaarabu.
Mwisho .
0 comments:
Post a Comment