Sunday, 11 August 2019

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari bin Zuberi Atoa Pole Kwa Wafiwa na Majeruhi Ajali ya Moto Morogoro

...
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari bin Zuberi ametoa salamu za pole kwa Rais, wafiwa na wote walioguswa na msiba kufuatia ajali ya moto mkoani Morogoro na kuagiza BAKWATA mkoa wa Morogoro kutoa ushirikiano wote utakaohitajika katika kipindi hiki.

Ajali hiyo imetokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019   baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta hayo.

Wakati huohuo, Sheikh Abubakari bin Zuberi  amesema swala ya sikukuu ya Eid Agosti 12,kitaifa itaswaliwa katika kiwanja cha Masjid Kibadeni Chanika ikifuatiwa na baraza la Eid na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger