Monday, 19 August 2019

MBUNGE WA IKOLOMANI APATA AJALI

...
Mbunge wa Ikolomani,Bernard Shinali amepata  ajali ya barabarani siku ya Jumapili, Agosti 18,2019 asubuhi wakati akisafiri kutoka Kakamega akielekea jijini Nairobi baada ya kuhudhuria hafla ya mazishi ya mwanawe wa kiume iliyofanyika Jumamosi

Shinali alikuwa akisafiri jijini Nairobi pamoja na watu wengine wanne wa familia yake wakati gari lake liligongana na matatu, eneo la Lessos kwenye barabara ya Kapsabet -Mau Summit.

Gari hilo lilikuwa limewabeba watu wengine wanne ambao walinusurika na wanapania kuendelea na safari yao baada ya kuandikisha taarifa kwa polisi.

 Hata hivyo, mbunge huyo alithibitisha kuwa familia yake pamoja naye wako salama salimini kupitia njia ya simu.

 Mwanasiasa huyo alikumbana na ajali hiyo wakati alikuwa akielekea jijini Nairobi baada ya kuhudhuria mazishi ya mwanawe wa kiume Chris Masakah, ambaye alikufa maji siku ya Ijumaa, Julai 26, katika jimbo la Arizona, nchini Marekani. 

Masakah alikuwa akihudumu katika jeshi la Marekani kama mwanamaji. 
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger