Monday, 19 August 2019

Mahakama yaamuru ushahidi wa video kesi ya Freeman Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA Uonyeshwe

...
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru kuonyeshwa kwa video iliyopokelewa mahakamani hapo kama ushahidi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ionyeshwe .

Uamuzi huo umetolewa  Agosti 19, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, baada ya kupitia hoja za upande zote mbili.

Uamuzi huo unatokana na upande wa utetezi kupinga video hiyo isionyeshwe mahakamani hapo kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuandaa mazingira wezeshi.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Simba alisema sababu zilizotolewa na upande wa utetezi haina mashiko, hivyo video hiyo inatakiwa ionyeshwe katika ukumbi wa Tehama uliopo katika mahakama ya Kisutu.

Hata hivyo hakimu huyo ameiairsha  kesi hiyo kwa muda wa dakika 20 kwa ajili ya maandalizi ya kuangalia video.

Video hiyo inayosemekana ilirekodiwa wakati wa ufungaji wa kampeni za uchaguzi mdogo  wa ubunge wa Kinondoni kwa tiketi ya Chadema Februari 16 mwaka 2018, inadaiwa kubeba matukio yanayomuonyesha Mbowe na wenzake tisa wakiwa kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi huo, na kwamba ina uhusiano na kesi hiyo.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger