
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Shedrak Mohamed
Vijana wilayani Kyerwa mkoani Kagera wametakiwa kuwa wabunifu katika masuala mbali mbali ya kiuchumi kuliko kusubiri ajira kutoka serikalini.
Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 13,2019,na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Shedrak Mohamed katika mwendelezo wa wiki ya uwekezaji Kagera yenye lengo la kutangaza fursa za mkoa wa Kagera.
Mohamed amesema vijana wanatakiwa kubuni na kutambua vipaji walivyonavyo kuliko kukaa bila kazi huku baadhi wakisubiri ajira kutoka serikalini.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa katika wilaya yake ya Kyerwa kipaumbele ni kwa vijana ili kujenga taifa imara na lenye nguvu.
Amesema vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali za mikopo zinazotolewa na halmashauri.
0 comments:
Post a Comment