Sukari ( Ya Kupanda ) ni tatizo linalo wasumbua na kuwatesa mamilioni ya watu duniani.
Habari njema ni kwamba zipo dawa mbalimbali za asili ambazo zina uwezo mzuri tu wa kushusha sukari iliyo panda sambamba na kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu kwa ufanisi mkubwa.
Kati ya dawa hizo zipo zinazo shusha sukari taratibu na zipo zinazo shusha sukari kwa haraka sana.
Mada yangu ya leo inahusu dawa za asili ambazo zinashusha sukari kwa haraka sana na tahadhari ya kuchukua kwa mtu anae taka kutumia dawa hizo.
Mtu mwenye tatizo la sukari ya kupanda anapokuwa anatumia dawa za asili kwa ajili ya kutibu tatizo lake anatakiwa kujua aina ya dawa anazo tumia.
Anatakiwa kujua kama dawa anayo tumia inashusha sukari kwa taratibu au inashusha kwa haraka.
Kwa dawa za asili zinazo shusha sukari kwa taratibu mhusika anaweza kuwa anatumia dawa usiku na mchana na kwenda kupima sukari kila baada ya wiki ili kujua sukari yake imepungua kwa kiasi gani. Hizi hazina risk sana kwa sababu zinashusha sukari kwa taratibu. Mhusika kulingana na kiwango cha sukari alicho nacho anaweza kutumia dawa zilizopo katika kundi hili kwa muda wa kuanzia mwezi mmoja hadi miezi mitatu kulingana na dawa husika.
Lakini kwa dawa zinazo shusha sukari kwa haraka, mhusika anatakiwa kuwa karibu sana na kipimo cha sukari ( Blood Sugar Test Kit )
Hii ni kwa sababu mhusika anatakiwa kuwa anapima sukari yake kila siku. Yani akitumia dawa usiku basi asubuhi atatakiwa kupima sukari yake ili kujua imeshuka kwa kiwango gani na akitumia asubuhi anatakiwa kupima tena usiku ili kujua sukari imeshuka kwa kiwango gani.
Kwa sababu asipo fanya hivyo sukari inaweza kushuka sana ( below normal ) jambo linalo weza kumsababishia madhara makubwa kwa sababu sukari below normal ni hatari sana kwa mhusika.
Asubuhi kabla haujala chakula sukari inatakiwa kuwa 4 na baada ya kula chakula inatakiwa isizidi 7. Sasa akitumia dawa zikashusha sana sukari yake ni risk kubwa sana kwake kwa sababu sukari ikiwa chini ni hatari sana.
Lakini akiwa na kipimo cha sukari ni rahisi kwake kujua sukari imefikia kiwango gani jambo ambalo litamuepusha na kuendelea kutumia dawa ya kushusha sukari wakati sukari yake tayari imekuwa normal.
Ndio maana tunasema mtu anae tumia dawa za asili kwa ajili ya kushusha sukari anatakiwa ajue dawa anazo tumia zipo kwenye kundi gani.
Kwa ushauri na kujua aina ya dawa za asili za sukari ambazo zinashusha sukari kwa haraka pamoja na zile ambazo zinashusha sukari kwa taratibu, wasiliana na duka la kuuza dawa za asili la NEEMA HERBALIST. Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM kwa namba 0693 005 189.
Tutembelee kwenye tovuti yetu : www.neemaherbalist.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment