Wednesday, 31 July 2019

Waziri Mkuu Majaliwa Akagua Maandalizi Ya Mapokezi Ya Wajumbe Wa Mkutano Wa Sadc Kwenye Kiwanja Cha Ndege Cha Julius Nyerere

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua jengo la tatu la abiria kwenye kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere ili kuona maandilizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano wa SADC.

Akizungumza na watendaji wa Serikali pamoja na Kamati ya maandalizi uwanjani hapo leo jioni (Jumatano, Julai 31, 2019), Waziri Mkuu amesema maandalizi ni mazuri isipokuwa kwa kasoro chache zilizobakia.

“Nimepita VIP hakuna shida. Pale terminal 2, sehemu ya Uhamiaji iko vizuri, uchunguzi wa afya nayo iko vizuri, lakini vyoo inabidi vibadilishwe haraka sana. Vile vyoo pale nje vimechoka, vibadilishwe mara moja, siyo tu kwa ajili ya ugeni, bali ni kwa faida yetu pia,” amesema huku akimwagiza meneja wa uwanja huo, Bw. Paul Lugasha aharakishe zoezi hilo.

Katika jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo, Waziri Mkuu amekagua eneo ambalo viongozi wakuu wa nchi watashukia, watakagua gwaride la heshima na kuangalia vikundi vya ngoma. Pia amekagua vyumba ambavyo watapumzikia kabla ya kuelekea mjini.

Amesisitiza kuwa usafi wa barabarani bado hauridhishi sababu kuna mawe, udongo na michanga kwenye barabara kuu ya kutoka uwanja wa ndege hadi mjini. “Tulikubaliana kuwa zile bustani ziboreshwe, vyuma vya barabarani vitengenezwe lakini hata leo nimepita kwenye fly-over, bado kuna mawe na michanga, hata sijui vinatokea wapi,” alisema.

Amewataka wahusika waweke banners za kutosha za aina mbalimbali na picha za wanyama kutani, uwanjani hapo ili kuonesha kwamba kuna mkutano mkubwa unafanyika hapa nchini.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka Watanzania watumie fursa ya uwepo wa mkutano huo mkubwa kuendesha biashara zao na ujasiriamali.

“Ziko fursa nyingi za uwepo wa mkutano huu. Kila mmoja atumie nafasi hii kuweza kuongeza na kuboresha kazi yake inayomletea uchumi,” amesema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,       
JUMATANO, JULAI 31, 2019.


Share:

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Awataka Wadau Wa Mazingira Kutekeleza Sheria,kanuni,na Taratibu Za Mazingira.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
MAKAMU wa Rais SAMIAH SULUHU HASSAN amewataka wadau wa mazingira kutekeleza Sheria,Kanuni na maandiko ili kuhimiza utunzaji wa rasilimali misitu na kurahisisha upatikanaji wa rasilimali za maji. 

Akizindua jukwaa la maendeleo endelevu kuhusu usimamizi bora wa misitu kwa upatikanaji wa rasilimali maji endelevu leo jijini Dodoma Makamu wa Rais amesema misitu ndio chanzo kikubwa cha rasilimali maji hivyo isipotunzwa na kusimamiwa vizuri watakuwa wanahatarisha upatikanaji wa maji kwa matumizi ya kijamii,kibiashara na kuimarisha mazingira. 

Ametaja mambo yanayosababisha athari kubwa kwa uhai wa rasiliamli maji kuwa ni kilimo kisichokuwa endelevu,ujenzi holela,uchomaji mkaa,ukataji kuni,uvunaji haramu wa magogo na ufugaji usiozingatia kanuni. 

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira GEORGE SIMBACHAWENE amesema haridhishwi na hali ya mazingira ilivyo na kuwataka wadau hao kupeleka fedha katika mazingira yanayoharibika badala ya kutumia kwenye makongamano. 

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Dodoma dokta BINILITH MAHENGE amesema ni vyema jamii ikijikita katika kulinda na kutunza mazingira na kwa viongozi kutekeleza yale wanayoazimia. 

Naye mkuu wa taasisi ya uongozi profesa JOSEPH SEMBOJA amesema  sekta ya maji na misitu ni muhimu hivyo ni vyema sera, mikakati na taasisi zinazohusu sekta hiyo  zikafungamana ili ziweze kufnaya kazi kwa ufanisi.
 
Jukwaa la maendeleo endelevu lilianzishwa mwaka 2012 ili kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya maji na misitu ili waweze  kujadili mpango wa maendeleo endelevu.


Share:

KISANDU ACHAGULIWA KUWA NAIBU MEYA MANISPAA YA SHINYANGA




Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga John Kisandu

Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga

Diwani wa Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga John Kisandu (CCM) amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, na kumshinda mpinzani wake Zena Gulamu (Chadema).


Uchaguzi huo wa Naibu Meya umefanyika leo Julai 31,2019 kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la madiwani wa kumchagua Naibu Meya pamoja na Kamati mbalimbali, ambazo zitasimamia utekelezaji wa maendeleo ya Manispaa hiyo, ikiwamo kamati ya fedha ya kudumu, uchumi, elimu na afya, miundombinu, ukimwi, maadili pamoja na Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT).

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, amesema John Kisandu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameibuka mshindi kwa kupata kura 15, dhidi ya mpinzani wake Zena Gulam kutoka Chadema ambaye amepata kura tano ,ambapo wajumbe waliopiga kura walikuwa 20.

Akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo, Kisandu ameomba ushirikiano kutoka kwa madiwani hao na kuwa kitu kimoja katika kuisimamia halmashauri kwa maslahi mapana ya wananchi na kuwaletea maendeleo.

Aidha madiwani hao wameendelea kujadili ajenda mbalimbali zikiwamo za afya, elimu, maji, miundombinu, fedha, kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya manispaa hiyo.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Diwani wa Kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM John Kisandu, akiomba kuchaguliwa kuwa Naibu Meya kwa mara nyingine tena, ambapo alishinda kiti hicho kwa kura 15.

Diwani wa viti wa maalumu Manispaa ya Shinyanga Zena Gulamu kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema(, akiomba kuwa naibu meya wa manispaa ya Shinyanga, ambapo alipata kura tano.

Madiwani wakipiga kura kumchagua Nibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga.

Upigaji kura ukiendelea.

Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga.

Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga.

Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga.

Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga.

Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu akijipigia kura ya kuchaguliwa kuwa Naibu Meya kwa mara nyingine.

Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akimtangaza diwani wa Kata ya Chibe John Kisandu kuwa mshindi wa Kiti cha Unaibu Meya kwa mara nyingine.

Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho tena, na kuwataka madiwani kushirikiana kwa pamoja kusimamia maendeleo ya halmashauri.

Madiwani wakiendelea na baraza mara baada ya kumaliza kuchaguzi wa Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga na wajumbe wa kamati mbalimbali.

Madiwani wakiendelea na baraza.

Baraza la madiwani likiendelea.

Baraza la madiwani likiendelea.

Diwani wa Kata ya Kitangili Hamisi Ngunila (CHADEMA), akizungumza kwenye baraza hilo.

Diwani wa Kata ya Ndala Wiliamu Shayo(CHADEMA) akizungumza kwenye baraza.

Baraza likiendelea.

Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani.

Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani.

Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu, akifunga mkutano wa mwaka wa baraza la madiwani na kuwataka watendaji na madiwani kila mtu awajibike kwenye nafasi yake ili kuleta maendeleo kwenye manispaa hiyo.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

Call for Papers: UNESCO Regional Conference on Africa 2019 – Accra, Ghana (Funded)

Call for Papers: UNESCO Regional Conference on Africa 2019 – Accra, Ghana (Funded), Call for Abstracts – Assessing challenges and opportunities towards effective governance of diversity in Africa. UNESCO is opening a call for abstracts in preparation of a Regional Conference on the theme: Governance of Diversity: Challenges and Opportunities for Sustainable Development and Peaceful Coexistence in Africa,… Read More »

The post Call for Papers: UNESCO Regional Conference on Africa 2019 – Accra, Ghana (Funded) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wananchi 144 Jijini Dodoma Wakabidhiwa Hatimiliki Kwa Masharti Nafuu.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amekabidhi hati ya viwanja kwa wananchi 144 wa Kata ya Tambukareli ambao maeneo yao yalitwaliwa na Serikali.

Kunambi amekabidhi hati hizo leo Julai  31,2019  kwa wananchi hao ambao wamekuwa wakihangaika takriban miaka mine hadi sasa. 

 Kunambi amefafanua kuwa  Halmashauri ya Jiji la Dodoma itahakikisha kila Mwananchi anapata haki yake kama ambavyo Rais Dk John Magufuli amekuwa akisisitiza kuwatetea wanyonge.

” Leo hii hapa kuna zoezi la kutoa viwanja kwa wananchi ambao ni wahanga wa maeneo yao ambao awali inadaiwa yalitwaliwa na iliyokua mamlaka ya ustawishaji Makao makuu na kuwaacha ndugu zetu hawa wakiwa hawana maeneo.

” Kwa muda mrefu kumekua na malalamiko ya muda mrefu ya wananchi na sisi kama Jiji tulifanya tathimini ya jumla na kuona ndugu zetu hawa wana haki ya kulipwa fidia maeneo yao na hivyo leo tumemaliza kero yao ya muda mrefu kwa kuwagaia viwanja bure na watakacholipia wao ni zile tozo za kawaida za kikatiba,” amesema Kunambi. 

Kunambi amesema katika mwaka  2018 wa Fedha tayari wameshatoa hati miliki 5000 na kuwa Jiji la kwanza Nchi nzima ikifuatiwa na Ilemela jijini Mwanza
.
” Ili tuweze kumaliza matatizo yote Dodoma basi Jiji linapaswa kutoa viwanja kwa mtindo huu wa leo kwa viwanja 5000 ambavyo vitatugharimu Shilingi Bilioni nne kwa hali ya kawaida sawa na kujenga vituo    vya afya 8. 

” Leo hii hawa wananchi ambao wako 144 tumewapa viwanja bure kwa maana watalipa tu zile gharama za kisheria takribani laki saba kwa kiwanja ambacho angeweza kulipa Shilingi Milioni saba. Hii ni kuonesha jinsi gani Serikali ya Dk Magufuli inatetea haswa wanyonge,” amesema Kunambi. 

Hata hivyo Kunambi amesema badala  ya Mwananchi kutoa gharama ya Tsh. milioni saba  anapunguziwa na kutoa  Laki saba pekee  kwa kiwanja na utoaji wa fedha hizo ni kwa masharti nafuu kutoa kwa awamu ndani ya miezi 6.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Juma Mazengo akizungumza kwa niaba ya madiwani    jiji la Dodoma amemshukuru Mkurugenzi wa Jiji kwa namna alivyolivalia njuga suala lao na kuweza kumaliza kero ya wananchi wake ambao wameteseka kwa miaka minne.

” Nimshukuru Mhe Rais kweli tumeona jinsi gani anatetea wanyonge. Hii inaonesha jinsi gani anaziishi ahadi zake alizowaahidi wananchi wakati wa kampeni, tunayo furaha sana na hakika tumeona heshima tuliyopewa na Serikali yetu,”amesema Mhe. Mazengo.


Share:

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo

SUPER MORISIS; nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa muundo wa vidonge na unga  , Huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-85)   Inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii)  inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa  tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya maratatu (3)bila hamu kuisha wala kuhisi kuchoka na  itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 18-45

SUNUPER;   Hurefusha na kunenepesha maumbire madogo ya uume uliosinyaa ,  matatizo haya huchagizwa ama husababishwa na tumbo kuunguruma na kujaa gesi hatimae kinyesi kuwa km cha mbuzi, ngili, kisukari, presha korodani moja kuvimba au kuingia ndani nk yote haya yanatibika kabisa na kupona kwa mad mfupi sana,

Pia nidawa ya vidonda vya tumbo miguu kuwaka moto na kupata nganzi, maumivu ya mgongo na kiuno 

ONDOA MATATIZOYAKO YOTE  ninadawa ya uzazi kwa pandezote mbili, kupunguza unene kitambi ( nyama uzembe)        kuondoa makovu mwilini, kuzuia mimba kuharibika,kusafisha nyota,  kuzuia majini wachafu, pete ya bahati,  kurudisha mali iliyopotea au kuibiwa 

Kwahuduma na msaada wasiliana na DR. GALIMBO  0759208637   /  0620510598


Share:

MUONEKANO WA DARAJA LA RELI YA KISASA YA SGR ENEO LA SHAURIMOYO JIJINI DAR ES SALAAM


Muonekano wa sehemu ya Daraja la Reli ya SGR litalopita juu kutoka Ilala hadi Stesheni ya Dar es salaam linavyoonekana likimaliziwa kujengwa maeneo ya Shaurimoyo kama lilivyopigwa picha leo na Issa Michuzi
Share:

Makusanyo Ya Kodi Kwa Kipindi Cha Mwaka Wa Fedha 2018/19

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya TZS 15.9 trilioni kati ya lengo la TZS 18 trilion kwa mwaka wa Fedha 2018/19 kuanzia tarehe 1 Julai 2018 hadi 30 Juni 2019. Aidha katika robo ya nne ya mwaka huo wa fedha yaani, mwezi Machi hadi Juni 2019, TRA ilikusanya TZS 1.1 trilioni, TZS 1.2 trilioni, na TZS 1.5 trilioni kwa mwezi Aprili, Mei, na Juni, mtawalia. Kwa namna ya kipekee kabisa, TRA inawashukuru walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kwa ushirikiano.

Ikumbukwe kwamba, katika mwaka huo wa fedha, Serikali ilianzisha Mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETS) ambao utekelezaji wake umefanyika kwa awamu mbili (2). Awamu ya kwanza, ilihusisha bidhaa za sigara, mvinyo, pombe kali, bia na aina zote za vileo. Awamu hii ya kwanza iliyoanza kutekelezwa tarehe 15 Januari 2019 imeendelea vizuri na maandalizi ya awamu ya pili ya utekelezaji wa ETS inayojumuisha bidhaa za vinywaji baridi, maji, juisi, na CD/DVDs yamekamilika. Hivo mfumo huu wa ETS kwa awamu hii ya pili, unatarajiwa kuanza kazi rasmi tarehe 1 Agosti, 2019.

Lengo kuu la kubandika stempu hizi za kielektroniki ni kuongeza usimamizi na ufanisi wa ukusanyaji wa Ushuru wa bidhaa ikiwa ni pamoja na kupata taarifa sahihi za uzalishaji viwandani ili kukusanya mapato stahiki.  

Ni matumaini ya TRA kuwa, wazalishaji, waingizaji, wasambazaji, wauzaji wote wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa pamoja, na umma kwa ujumla wataendelea 
kutoa ushirikiano kwa TRA ili kufanikisha utekelezaji wa mfumo huu kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Richard M. Kayombo
KAIMU MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI


Share:

MKUU WA MKOA WA MARA AZINDUA KAMPENI YA 'NYUMBA NI CHOO'

Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima

Na Asha Shaban - Mara
Zaidi ya kaya 22,540 zinadaiwa kuwa na ukosfu wa vyoo bora katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara jambo ambalo linafanya kaya hizo kujisaidia sehemu zisizo rasmi ikiwemo ndani ya Ziwa Victoria.

Kufuatia kuwepo kwa idadi kubwa za kaya kukosa vyoo mkuu wa mkoa wa mara Adam Malima alitoa agizo la muda wa siku 60 kwa wakazi wote wa mkoa huo ambao hawana vyoo kujenga vyoo hivyo ili kuepuka maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.

Akizindua kampeni ijulikanayo kama nyumba ni choo kampeni inayolenga kuhamasisha matumizi ya vyoo katika jamii mjini hapa jana Mkuu wa mkoa alisema kuwa ni aibu kubwa kwa wakazi wa mkoa huo kushindwa kujenga vyoo na kuvitumia ipasavyo katika zama hizi na kwamba atakayeshindwa kutekeleza agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Mbali na kutoa muda huo lakini pia Mkuu huyo wa mkoa aliwaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani humo kutoa taarifa ya upatikanaji na matumizi ya vyoo bora kila baada ya miezi mitatu lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa vyoo bora vinakuwepo kutumika ipasavyo muda wote.

Malima aliwataka wakazi wa mkoa wa Mara kuachana na mila potofu ambazo ni miongoni mwa sababu zinazochangia matumizi hafifu ya vyoo huku akifafanua kuwa zipo baadhi ya jamii ambazo baba anashindwa kutumia choo kimoja na watoto pamoja na wanafamilia wengine hivyo kusababisha kaya kukosa choo

Awali Afisa afya wa mkoa wa Mara, Dk. Bumija Mhando alisema kuwa hadi Desemba 2018 ni asilimia 55 tu ya kaya za mkoani Mara ndiyo zenye vyoo bora huku asilimia 38 zikiwa na vyoo vya asili na asilimia saba zikiwa hazina vyoo kabisa.

Dk. Mhando Aliongeza kuwa takwimu pia zinaonyesha ni asilimia 6 tu ya wakazi wa Mara ndio wananawa mikono kwa maji safi na sabuni baada ya kutoka chooni jambo ambalo linahitaji jitahada zaidi kuhamasisha na kuelimsiha jamii juu ya umuhimu wa kunawa mikono mara baada ya kutoka chooni.

Naye Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano alisema kuwa anakusudia kuwachukukia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutoza faini kuanzia sh 20,000 kwa mkazi yeyote wa wilaya yake ambaye atashindwa kujenga na kutumia choo ipasavyo.

Alisema kuwa kufuatia kampeni iliyoendeshwa na serikali wilayani Musoma wakazi wengi wa wilaya hiyo waliweza kujenga vyoo huku changamoto kubwa ikiwa ni matumizi sahihi ya vyoo hivyo kwavile wapo baadhi yao wanajisaidia porini na ziwani.

"Sasa hivi tutaanza msako wa nyumba kwa nyumba kuangalia kama vyoo hivyo vinatumika kwavile tumegundua kuna vyoo vimejengwa kwaajili ya ukaguzi huku mkisema ni choo cha DC sasa nakuja kuangalia kama kweli hicho choo kinatumika au ni cha DC", alisema Naano.

Nyakwesi Majura ni mwananchi wa manispaa ya Musoma alisema katika mila yao hawawezi kushea choo moja na baba mkwe wake hivyo hata kama choo kupo basi kinakuwa hakitumiki kwa kuofia kuvunja miiko iliyopo ndani ya mila zao.

Alisema kuwa kwa sasa wanaanza kubadili tabia kutokana na elimu wanazo zipata na kujua madhara ya kujisaidia hovyo kuwa yanaleta magonjwa ya mlipuko na kuwa ni uchafuzi wa mazingira. 

Share:

Makerere University Mak Graduate Admission Lists for 2019/20 Academic Year

makerere graduate admission list 2019 admission list makerere university postgraduate admission list makerere university graduation list 2019 makerere university masters admission 2019 makerere university graduate admission 2019/20 makerere university admission list 2019/20 makerere university graduation list 2019 pdf

The Directorate of Research and Graduate Training (DRGT), Makerere University has released the admission lists for postgraduate applicants successfully admitted for the 2019/20 Academic Year. The lists include those of candidates admitted to eight colleges of Makerere University. Additional lists will follow.

Please see the Downloads below for admitted students listed by College.

For further enquiries please contact

The Directorate of Research and Graduate Training (DRGT),

Level 4 Senate Building
Makerere University
P.O. Box 7062 Kampala
Telephone: +256 (414) 691-937
Email: drgt[at]rgt.mak.ac.ug

DOWNLOADS & ESSENTIAL ATTACHMENTS

Attachment Size
PDF iconPDF icon

Makerere-DRGT-Graduate-Admission-Lists-2019-2020-CAES.pdf

767.99 KB
PDF iconPDF icon

Makerere-DRGT-Graduate-Admission-Lists-2019-2020-CoCIS.pdf

458.19 KB
PDF iconPDF icon

Makerere-DRGT-Graduate-Admission-Lists-2019-2020-CEES.pdf

569.6 KB
PDF iconPDF icon

Makerere-DRGT-Graduate-Admission-Lists-2019-2020-CEDAT.pdf

702.9 KB
PDF iconPDF icon

Makerere-DRGT-Graduate-Admission-Lists-2019-2020-CHUSS.pdf

832.5 KB
PDF iconPDF icon

Makerere-DRGT-Graduate-Admission-Lists-2019-2020-CoNAS.pdf

404.66 KB
PDF iconPDF icon

Makerere-DRGT-Graduate-Admission-Lists-2019-2020-CoVAB.pdf

298.74 KB
PDF iconPDF icon

Makerere-DRGT-Graduate-Admission-Lists-2019-2020-SoL.pdf

 

The post Makerere University Mak Graduate Admission Lists for 2019/20 Academic Year appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Maadhimisho Na Maonesho Ya Nne Ya Wiki Ya Viwanda Ya Jumuiya Ya Maendeleo Ya Kusini Mwa Afrika (SADC)




Share:

Wananchi Waishukuru TARURA baada ya kutatuliwa kwa kero yao ya muda mrefu kwa kujengewa Daraja la Chuma

 Na. Erick Mwanakulya
Wananchi wa Kata ya Chita Melela iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, wameshukuru Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) baada ya kutatuliwa kwa kero yao ya muda mrefu kwa kujengewa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi ambalo linajengwa na TARURA chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID).

Hayo yameelezwa na wananchi waliojitokeza kushuhudia ujenzi wa Daraja hilolinalojengwa na Wahandisi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),wakisaidiana na Mhandisi Mshauri Ebenezer Mollel pamoja na Mtaalamu wa UfundiJohn Hinderer kutoka Kampuni ya Mabey Bridge ya nchini Uingereza.

Wakielezea furaha yao juu ya ujenzi wa daraja hilo, wananchi hao wamesema kuwa wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwajengea daraja maana walikuwa wanapata shida kubwa hapo awali katika kusafirisha bidhaa zao na kupata huduma mbalimbali za kijamii kwani walikuwa wanatumia mtumbwi kuvuka Mto ambapo ni umbali takribani Km 1.5.

Kwaupande wake, Diwani wa Kata ya Chita Melela Mhe. Chelele John amesema, Serikali ya Awamu ya Tano inastahili kupongezwa kwa maana Daraja hilo ni kiungo muhimu katika uchumi wa Kata yake pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kwa maana vyanzo vya mapato katika Kata za Mlimba, Chita, Mgeta, Mangula pamoja na Mchombe vitakusanywa kwa urahisi kutokana na uwepo wa daraja hilo.

“Tulikuwa tunatumia mtumbwi kuvuka Mto na wananchi walipata adha kubwa katika Kijiji chetu kwani kufikia huduma za kijamii ilikuwa changamoto kubwa, leo hii naona Wahandisi wa TARURA wapo hapa katika ujenzi wa Daraja hili, hii inadhihirisha kuwa Wakala upo katika kuhudumia wananchi ipasavyo nasi tunawaunga mkono”, alisema Diwani huyo.

Naye, Mratibu wa TARURA Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Mpinzile amesema Daraja la Chuma (Mabey Bridge) la Mto Kihansi limewekwa baada ya kutengeneza barabara ya Chita Melela yenye urefu wa Km 11.5 na litakuwa mkombozi kwa wananchi wa Chita kutokana na shida wanayoipata wakati wa mvua na kwamba Wakala utaendelea kuikarabati Barabara hiyo hadi kuunganisha Kata ya Mlimba ili kuwarahisishia wananchi kufanya shughuli zao za kila siku.

Pia, amewasihi wakazi wa Chita kutunza miundombinu ya Barabara pamoja na Daraja kwani gharama kubwa zimetumika katika ujenzi wa Daraja hilo.

Daraja la kisasa la Chuma (Mabey Bridge) ambalo limegharimu zaidi ya shilingi milioni 700 ni moja kati ya kazi za Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika kuboresha Barabara na kufanya matengenezo pamoja na ujenzi wa Madaraja ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Daraja hilo linalenga kutatua kero ya kudumu kwa wananchi wa Chita Melela kutokana na Madaraja ya hapo awali kusombwa na maji pale mvua zinaponyesha na linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Muonekano wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro baada ya kukamilika kwa ujenzi wa awali ambapo uzinduzi rasmi wa Daraja hilo utafanyika hivi karibuni.
Daraja la awali la wananchi wa Kata ya Chita Melela lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, ambalo limekuwa likitumiwa na wakazi maeneo hayo kabla ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kutengeneza Daraja jipya la Chuma (Mabey Bridge) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID).


Share:

ONJA UTAMU WA 'JUISI LA JAMBO'........'SODA LA JAMBO'



Share:

Ombi la Rais Magufuli kwa kampuni ya ujenzi Njombe latekelezwa

Na.Amiri kilagalila-Njombe
Kampuni ya ujenzi wa barabara ya kichina China Henan international cooperation group co ltd (CHICO) inayotekeleza mradi wa barabara wa km 53.9 Njombe-Moronga kuelekea wilayani Makete mkoani Njombe.

Imeanza utekelezaji wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na bwalo moja la chakula katika shule ya msingi ramadhani mjini Njombe kutokana na ombi la Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliloomba wakati wa ziara yake april 10 mkoani hapo mara baada ya Rais Magufuli kuombwa na wanafunzi wa shule hiyo wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya  Njombe-Makete.

Waziri wa ujenzi Elias kwandikwa amefika na kukagua shughuli zinazoendelea katika ujenzi huo na kumshukuru mkandarasi kwa utekelezaji huo.

“Kwanza nimshukuru sana mheshimiwa Rais alivyoweza kulisukuma jambo hili na hatimaye tumepata huu mradi  lakini pia na hawa wenzetu wa Chico kwa haraka wameanza utekelezaji kwa kweli mimi ninashukuru sana”alisema Kwandikwa

Lusekelo kijalo ni injinia wa kampuni hiyo amesema ujenzi wa majengo hayo unategemewa kukamilika kabla ya mwezi mmoja na nusu kuisha huku ujenzi huo ukigharimu karibu milioni 240 pindi utakapokamilika

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Ephrahim sanga amesema mradi huo ni mkubwa katika shule hiyo kwa kuwa ina wanafunzi 1552 na kupelekea kuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa.

“Mimi hapa nina wanafunzi 1552 wavulana 648 na wasichana 604 vyumba vyetu vya madarasa ni vichache sana havitoshelezi,ingawa tulikuwa na mpango wa kujenga shule nyingine mpya lakini mh.Rais ametutangulia kwa kweli tunashukuru tukaona tuanzie hapa ili tuweze kuigawa shule pawe na mikondo miwili”amesema mwl.Sanga


Share:

JESHI LA POLISI LATOA UFAFANUZI KIFO CHA MTUMISHI WA WIZARA YA FEDHA


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ametolea ufafanuzi kifo cha mtumishi wa Wizara ya fedha, Leopard Lwajabe (56), ambaye mwili wake ulipatikana ukiwa umening’inia kwenye mti wa muembe katika kijiji cha Mgoza wilayani Mkuranga.

Mambosasa amesema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa eneo la tukio hakukuwa na viashiria vyovyote vya kujitetea wakati wa tukio na kwamba mwili wa marehemu hakukuwa na jeraha lolote isipokuwa shingoni kulikokuwa kumefungwa kamba iliyotumika kujingonga.

Ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano Julai 31, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema mnamo Julai 26 mwaka huu Polisi Kanda Maalum ya Rufiji walipokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mgoza, Mohamed Said (68), kwamba kumeonekana mwili wa mwanaume ukiwa unang’inia kwenye mti wa muembe na polisi walipofika waliukuta mwili huo ukionesha mhusika amenyinyonga.

“Julai 29, mwaka huu walipatikana ndugu wawili wa marehemu ambao ni Chumila Mwalimu mkazi wa Manyara na Jonathan Herman ambaye ni mfanyakazi mwenzake na marehemu ambao walifanikiwa kuutambua mwili na kueleza kuwa marehemu alitoka nyumbani kwake kwenda ofisini akiwa na dereva wake na baadae alimtuma dereva akamchukulie simu nyumbani kwake Kinyerezi na baada ya hapo marehemu alitoweka ofisini na kwenda kusikojulikana hadi alipogundulika amejinyonga,” amesema.

“Mnamo Julai 29, wafanyakazi waligundua kuwa marehemu aliacha notebook mezani kwake iliyokuwa na mgawanyo wa mali zake ambapo aliruhusu kati ya ng’ombe anaofuga wanne watumike katika msiba wake na pia simu aliyomtuma dereva iligundulika kuwa imeshafutwa kumbukumbu zote,” amesema.

Aidha amesema mwili wa marehemu ulihamishiwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na ilibainika kifo hake kilisababishwa kwa kujinyonga ambapo chanzo hakijafahamika mpaka sasa na upelelezi uaendelea.

“Mtu aliyeuawa mahali halafu akaeda kufungwa kuna vitu vinavyokosekana kwa mfano mtu anayejinyonga lazima aachie haja ndogo na kubwa kwababu ya nguvu ya roho kutoka na hivyo vyote vimekutwa aneo la tukio,” amesema Mambosasa.


Share:

Uhamiaji Yafunguka suala la Kushikiliwa Mwandishi Erick Kabendera

Na. Mwandishi Wetu.
Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji imetoa ufafanuzi kuhusu Mwandishi wa kujitegemea Erick Kabendera baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kuwa amekamatwa na anahojiwa kuhusu uraia wake na Idara ya Uhamiaji Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Uraia na Pasipoti wa Idara ya Uhamiaji Gerald Kihinga, amesema kuwa  Erick Kabendera ameshikiliwa na Jeshi la Polisi na Uhamiaji Jijini Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi ili kuweza kupata taarifa juu ya uraia wake.  
 
Kamishna huyo wa Uhamiaji amesema Idara ya Uhamiaji inadhamana kubwa ya kusimamia na kutekeleza Sheria ya uraia wa Tanzania sura ya 357 rejeo la 2002, inayotoa mamlaka kwa taasisi hiyo kuchunguza na kuthibitisha uraia wa mtu yeyote. 
 
“Idara ya Uhamiaji ni chombo kilichopewa dhamana kubwa ya kutekeleza na kusimamia uraia wa Tanzania, kwa hiyo siyo mara ya kwanza kufanya hivyo, sisi tunamshikilia Kabendera kwa mahojiano kuhusu uraia wake, na siyo yeye tu aliyefanyiwa hivyo, idara ya Uhamiaji inatimiza matakwa ya sheria ya uraia nchini na wala si vinginevyo” Alisema.  
 
Alieleza kuwa idara ya Uhamiaji ilipata taarifa za Erick Kabendera kutoka kwa raia wema na ikaamua kumtafuta ili kufanya naye maojiano lakini hakuwa tayari kutoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kukataa kufika ofisi za Uhamiaji, hali iliyopelekea kukamatwa na sasa anaendelea kuhojiwa.  
 
Mkuu huyo wa masuala ya uraia na Pasipoti alifafanua kuwa, kushikiliwa huko kwa Erick Kabendera na kuendelea na mahojiano ni swala ambalo limekuwepo kwa raia wote ambao uraia wao una utata, wakiwemo watu wa kawaida,  watu mashuhuri na wengine wowote ambao kutaonekana uhitaji.  
 
Amesema kumekuwa na ushirikiano baina ya Uhamiaji na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ikwemo Polisi, ili kutekeleza majukumu mbalimbali ya kiusalama kwa nchi hivyo kukamatwa kwa Kabendera siyo jambo geni bali Idara inatimiza majukumu yake chini ya Sheria ya uraia wa Tanzania sura ya 357 rejeo la 2002.


Share:

Korea Kaskazini Yafyatua Makombora Mengine Mawili

Korea Kaskazini imefyatua  tena makombora mawili ya masafa mafupi leo, ikieleza kuwa ni onyo kwa Korea Kusini dhidi ya mpango wake wa kufanya mazoezi ya kijeshi pamoja na Marekani. 

Korea Kusini imesema, makomobora hayo mawili yalirushwa kutoka eneo la Winsan la pwani ya mashariki majira ya alfajiri, na kuruka umbali wa kilomita 250 hadi baharini. 

Korea Kaskazini imepigwa marufuku kurusha kombora chini ya maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini hii ni mara ya pili kufanya hivyo katika kipindi cha wiki moja, licha ya mkutano kati ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un na Rais wa Marekani, Donald Trump mwezi uliopita. 

Marekani na Korea Kaskazini wamekuwa wakishiriki katika mchakato wa kidiplomasia wa muda mrefu, kuhusu mpango wa makombora wa Korea ambao umepelekea viongozi wa mataifa hayo mawili kukutana mara tatu tofauti katika mwaka mmoja.


Share:

MKUU WA WILAYA YA MISSENYI KANALI MWILA AONYA WANANCHI KUHIFADHI WAHAMIAJIA HARAMU

Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila  

Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog Bukoba
Mkuu wa wilaya ya Missenyi  mkoani Kagera Kanali Denice Mwila  amewataka wananchi wilayani Missenyi kuacha tabia za kuwapokea na kuwahifadhi wahamiaji haramu kutoka nchi jirani kwani tabia hizo zinaweza kuhatarisha usalama wa nchi.


Akizungumza na Malunde 1 blog leo Julai 31,2019 Kanali Mwila ametoa amesema vitendo hivyo vimekuwa vikisababisha wahamiaji haramu kuongezeka wilayani missenyi mkoani hapa  hivyo kupelekea watanzania kukosa ardhi ya kulima na kufanya shughuli za ufugaji.

Kanali Mwila amewataka Watanzania katika maeneo ya mipakani hususani kata za Mtukula,Kakunyu na Minziro waepuke kupokea rushwa kutoka kwa wahamiaji ili wawape hifadhi.

Ameonya kuwa serikali wilayani humo haitawafumbia macho wananchi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.


Share:

Tudu Lissu Kasema Kwa Sasa Kapona, Hatumii Tena Dawa wala Magongo

Mwanasheria Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Tundu Lissu amesema amehitimisha matumizi ya dawa alizoanza kuzitumia tangu Septemba 7 mwaka 2017.

Lissu alianza kutumia dawa hizo Septemba 7 mwaka 2017 baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa katika makazi yake Area D jijini Dodoma ambapo tangu wakati huo amekuwa akipatiwa matibabu nje ya nchi.

Katika salamu kwa marafiki zake alizozitoa leo Jumatano Julai 31, 2019, kupitia ukurasa wake wa Instagram,  Lissu ameandika;

 
Hello Marafiki wa Mimi,
Habari za masiku mengi. Sijawasemesha kwa kitambo kidogo. Nisameheni bure, nafikiri mnafahamu jinsi ambavyo mambo yamekuwa mengi. Nina mambo mawili, nayo ni mema tu. .

La kwanza linahusu hali yangu ya afya. Leo tarehe 31 Julai, 2019, ni siku ya kwanza tangu niliposhambuliwa Septemba 7, 2017, situmii dawa ya aina yoyote. .

Kwa maelekezo ya madaktari wangu, jana ilikuwa siku ya mwisho ya mimi kutumia madawa ambayo nimeyatumia tangu siku niliposhambuliwa. .

Na jana hiyo hiyo nilitimiza mwezi mzima tangu niache kutumia magongo. Ijapokuwa bado nachechemea kwa sababu ya goti kutokukunja sawa sawa, sasa ninatembea bila msaada wa magongo. .

Safari yangu, na yetu, ndefu ya matibabu itakamilika Agosti 20 nitakapokutana na timu ya madaktari wangu kwa ajili ya vipimo vya mwisho na ushauri. .

Baada ya hapo itakuwa ni maandalizi ya kurudi makwetu. Hakutakuwa na sababu tena ya kitabibu ya mimi kuendelea kukaa Ulaya. .

Kwa vile tumekuwa pamoja kwenye safari hii ndefu, hatuna budi kupongezana na kumshukuru Mungu kwa hatua hii nzuri nilikofikia. Mimi na familia yangu hatutachoka kuwashukuru sana kwa kuwa pamoja nasi katika kipindi chote hiki kigumu. Mungu awabariki sana. .

La pili linahusu ubunge wangu. Tangu Spika Ndugai anivue ubunge, sijasema maneno mengi sana, zaidi ya kusema kwamba tutaenda Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo. .

Kesi za ubunge, kama zilivyo kesi zote za uchaguzi wa kisiasa, ni kesi za kisiasa. Ni mwendelezo wa mapambano ya kisiasa katika uwanja tofauti. .

Kwa sababu hiyo, ni kesi nyeti na za kipekee sana. Zinahitaji umakini mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha. Nina uzoefu mkubwa nazo, kwa sababu nimezifanya sana tangu 2005. 
 
Sasa ninaweza kuwafahamisha kwamba mimi na timu ya mawakili wangu tuko tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania. Tutafanya hivyo muda wowote kuanzia leo. Maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika.
 
Tunataka kuiomba Mahakama Kuu itoe jibu la swali alilouliza Spika Ndugai na walio nyuma yake: je, Spika wa Bunge la Tanzania ana uwezo kikatiba na kisheria, wa kufuta ubunge wa mbunge yeyote yule, kwa sababu yoyote ile, bila kumuuliza mbunge husika jambo lolote kuhusu sababu za kumfuta ubunge huo??? .

Nitawajulisheni mara moja kesi hii itakaposajiliwa rasmi. Kama itawapendeza, nitawaomba mtakaopata nafasi kuhudhuria mahakamani, kwa niaba yangu, wakati wote kesi hiyo itakapokuwa inaendelea. .

Nilitaka kuwashirikisheni haya kwa leo. Nawashukuruni sana na Mungu awabariki sana.


Share:

MGEJA AMUOMBA WAZIRI MKUU KUITISHA MKUTANO WA WADAU WA MICHEZO NCHINI


 Mwenyekiti mstaafu wa chama cha soka mkoani  Shinyanga  (SHIREFA)  Khamis Mgeja  ambaye pia ni mdau mkubwa wa soka nchini amemuomba  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa kuitisha Mkutano wa wadau wa sekta ya michezo nchini ili  kujadili changamoto na mstakabali wa maendeleo ya michezo mbalimbali hapa nchini ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa na watu walio wengi.


Mgeja ambaye pia Kada wa Chama Cha Mapinduzi ambaye kwa sasa amejikita katika sekta ya michezo hususani ile ya kukuza vipaji kwa  Vijana waliopo Wilayani Kahama ameamua kumuomba Waziri Mkuu akiamini ni msikivu na Mwanamichezo mzuri na kuongeza kuwa kama itampendeza  na atakavyoona inafaa, afanye na yeye kuwaita wadau wa sekta ya michezo kama alivyofanya kazi nzuri Dkt. John Pombe Magufuli alipowaita na kukutana na wadau wa sekta nyingine hapa nchini.

Mwenyekiti huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari leo Julai 31,2019 Mjini Kahama na kuhusu mustakabali wa soka letu la Tanzania hususani katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ambayo timu yetu ya taifa imeshiriki kuanzia ile ya chini ya miaka 17 pamoja na ile ya wakubwa ya kombe la mataifa ya Afrika sambamba na michuano hii ya kombe la Mataifa ya Afrika  kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

Alisema Michezo kwa sasa ndiyo inachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi pamoja na kuoa ajira kwa makundi makubwa ya Vijana ambao kwa sasa ndio makundi makubwa ambayo yapo mitaani hayana ajira za kudumu na kupitia michezo wanaweza kujiajiri na kujipatia fedha zitakazokuza maisha yao ya kila siku.

Mgeja alisema kuwa katika siku za hivi karibuni Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliitisha Mikutano kwa nyakati tofauti zikiwahusisha wadau kama vile  wa madini na baadae wafanyabiashara, vikao hivyo tuliona vilikuwa na tija mafanikio makubwa katika ujenzi wa Taifa. Baada ya wadau kupata nafasi ya kusema changamoto na mafanikio.

Aidha alisema mkutano huo wa sekta ya michezo kama utaitishwa utatoa fursa ya wadau mbalimbali kutoa michango yao ya kimawazo na  kujadili jinsi gani tutoke hapa tulipo kwenye aibu za mara kwa mara ili twende na kufika kwenye faraja hali ambayo tutapata wadau wengi na ikiwezekana wakawa na mawazo  mazuri tofauti tofauti tukabadilishana mawazo na uzoefu na kufikia muafaka na kupanda daraja la michezo.

Hata hivyo  Mgeja aliwaomba Watanzania hasa  wadau wa michezo wavute subira pamoja na kwamba tumeumia sana na tunaendelea kuumia baada ya matokeo ya mashindano ya watoto chini ya umri wa miaka 17 Afcon yaliyofanyika nchini kwetu na baadae Afcon ya wakubwa Misri hatuna sababu ya kutafuta mchawi wala kumtoa mtu kafara haitatusaidia chochote kuleta mabadiliko ya michezo na kama hatutajielekeza kuwekeza katika michezo Tanzania tutaendelea kuwa washiriki na wala shio washindani na tusitarajie kuvuna bila kupanda kama matunda pori.

Mwenyekiti huyo Mstaafu wa Chama cha soka Mkoani Shinyanga alisema kuwa hakuna njia ya mkato katika mafanikio yoyote yale bila kuwekeza tatizo letu sie watanzania tunataka matokeo mazuri kitu ambacho hakiwezekani hata ukitaka pepo lazima ufe kwanza.

“Msitake pepo bila kufa na inasikitisha tunataka maendeleo bila kuwekeza katika shule za mpira za watoto wadogo hapa nchini na hakuna njia nyingine yeyote ya kupata mafanikiom katika soka bila ya kuwea na shule za kufundisha watoto tangu wakiwa wadogo mapka wanapokuwea wakubwa na kusajiliwa na vilabu vingine”,alisema Mgeja.

Mgeja pia amewapongeza wachezaji na kocha wao Amunike kwa pale walipofikia ni kweli vijana wetu uwezo wao ndipo ulipofikia katika mashindano ya Afcon na Misri ukweli utabaki pale pale. Ni kujidanganya kuwa tungeweza kufika kwenye  robo fainali au nusu fainali na hatimaye fainali hayo yangekuwa maajabu makubwa ya dunia .

Alisema tumejifunza kuanzia Afcon ya watoto na wakubwa Misri tumeona wenzetu Nchi zingine walivyowekeza kwa kiwango cha juu sana katika Academy Nchi kama Madagasca  na Burundi na mfano wa kuigwa na sisi tujipange upya naimani tutafika pazuri penye faraja na sasa tumeingia katika mashindano ya Afcon ya wachezaji wa ndani na watanzania wanapenda kuona mabadiliko makubwa katika soka letu.

Alisema kuwa michezo kwa sasa hapa Duniani ndio chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana ikiwa ni pamoja na kujenga afya za mwili na kama serikali itaongea na wadau mbalimbali kama ilivyo kwa sekta nyingine kunaweza kukaleta mabadiliko makubwa na hivyo kufanya nchi yetu kukua kwa kiwango cha juu katika sekta ya michezi kama ilivyo kwa nchini nyingine barani Afrika.

Mgeja pia aliwapongeza ushirikiano mkubwa kama Taifa ulivyooneshwa katika mashindano ya Afcon chini ya umri wa miaka 17 yaliyofanyika Nchini na Afcon ya wakubwa tuliyoshiriki Misri, Ushirikiano wa pamoja wa hali na mali ukiongonzwa na Mhe Rais Dr. John  Magufuli, Makamu wa Rais ,Waziri mkuu, Waziri wa michezo viongozi wa TFF, Mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji Taifa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Wadhamini mbalimbali wasani na Watanzania wote  kwa ushirikiano huu tuliouonesha tunaweza kupiga hatua kubwa ya mafanikio kama walivyofanya nchi zingine Mfano Aljeria, Everycost, Cameroon, Nigeria, Misri, Tunisia na Senegal.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger