Monday, 17 June 2019

SIMBA SC YAMPIGA PINGU KAGERE

...
MFUNGAJI Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kueendelea kuitumikia klabu ya Simba.
Kama kawaida, Simba SC mchana wa leo imemtambulisha mchezaji iliyemsajili na kwa mara nyingine imeendelea kuwapa mikataba mipya wachezaji wake waliokuwepo kwenye kikosi cha msimu uliopita.

Uamuzi wa Simba kumuongezea mshambuliaji wake Meddie Kagere miaka
Miwili umeelezwa umetokana na mambo mawili makubwa.

MOJA:
Ni baada ya Kagere raia wa Rwanda kufanya vema msimu uliopita akiibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara. Hivyo Simba wameona makali yake bado wanayahitaji.


MBILI:
Simba imeona idadi ya timu zinazomfuatilia Kagere kutaka kupata saini yake zimeongezeka.


Hadi timu kubwa kama Al Ahly, Zamalek nazo zimeonyesha nia na Simba walichofanya ni kumpa mkataba na baada ya hapo ni tusubiri atakayemtaka amwage mamilioni.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger