Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili waliofahamika kwa majina ya 1. JAPHET YAHAYA NGUKU [37] na ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa miaka sita [06] aitwaye ROSE JAPHET Mkazi wa Kijiji cha Msewe, Wilayani Mbarali.
Ni kwamba mnamo tarehe 03.05.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Kijiji cha Msewe kilichopo Kata ya Igurusi, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya katika msitu wa hifadhi wa Chimala Mtoto aitwaye ROSE JAPHET [06] alikutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na kukatwa kanyagio la mguu wa kulia ambapo kanyagio la marehemu limekutwa limefukiwa huko Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Chanzo cha tukio hili ni tamaa ya kupata utajiri ambapo baba mzazi wa marehemu aitwaye JAPHET YAHAYA NGUKU alimtoa mwanae kwa ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA ambaye ni mfanyabiashara kwa malipo ya Tshs 5,000,000/= ili auwawe na kisha kukatwa kanyagio la mguu wa kulia na kupatiwa mfanyabiashara huyo ili apeleke kwa mganga ili amtengenezee ndagu (dawa ya utajiri) ili afanikiwe katika biashara zake za Shule anayoimiliki iitwayo HAPPY iliyopo Mbalizi.
Mfanyabiashara huyo ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA amekiri kuhusika na tukio hilo. Ufuatiliaji unaendelea ikiwa ni pamoja na msako mkali wa kumtafuta mganga huyo kwa hatua zaidi za kisheria.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
0 comments:
Post a Comment