WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amezitaka halmashauri kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya visanduku vya huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu katika shule zote za msingi na sekondari.
Pia amesema ni lazima wakurugenzi katika halmashauri zote kuwa na visanduku huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu na mengineyo katika ofisi zao jambo ambalo litawasaidia wafanyakazi wenye matatizo hiyo kupewa huduma ya kwanza kabla ya kufika hospitalini.
Jafo alitoa maagizo hayo jijini hapa baada ya maandamano ya kuadhimisha Siku ya Pumu Duniani ambayo huadhimishwa Mei 7 kila mwaka.
Alisema tatizo la pumu ni kubwa na takwimu zinaonesha kuwa nusu ya watu wenye pumu ni watoto ambao wengi wako mashuleni na hawana uwezo wa kujisaidia.
“ Ukiangalia takwimu za Shirikala afya zinasema vifo vinavyotokana na pumu hapa nchini ni zaidi ya 2,000, sasa kama nusu ya hao ni watoto hii inamaanisha tunapoteza shule mbili nzima, yaani wanafunzi wa shule iliyokamili kutoka Darasa la Kwanza hadi la Saba. Hii inaonesha tatizo hili ni kubwa na kama taifa tunahaja ya kutathimini kama taifa.”
Kutokana na hali hiyo, Jafo aliagiza halmashauri katika bajeti ya mwaka 2020/2021, halmashauri zitenge fedha Sh laki 100,000 kwa kila shule katika eneo lake ili kununua visanduku viwili vya huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu.
“ Ghamara ya first aid kit moja ya huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu ni Sh 50,000 hivyo kila shule ikitengewa kits mbili haitakuwa fedha kubwa, Hivyo kwa shule zote zaidi ya 17,000 kutenga Sh bilioni 1.7 kwa hili sio fedha nyingi. Maadamu bajeti imeshipata, tutakapoanza maandalizi ya bajeti nyingine, halimashauri iliingize hili.”
Jafo alisema jamii kubwa ya Watanzania haina ufahamu wa tatizo la ugonjwa wa pumu, dalili na namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa wa aina hii hivyo aliwataka maadhimisho hayo kupewa kipaumbele kwa Waganga wakuu wa mikoa na wilaya katika maeneo yao kuadhimisha siku hii kwa kutoa elimu katika jamii na mashuleni.
Pia aliaziagiza halmashauri na mipango miji kutenga maeneo kwa ajili ya mazoezi ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukizo, akiutaka mkoa wa Dodoma kuangalia namna ya kutenga siku moja kwa mwezi kwa walimu na wanafunzi kushiriki katika mazoezi
Jafo pia alisema kwa kushikiana na wizara nyingine wataangalia namna ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhudumia magonjwa yasiyoambukiza na kuangalia namna ya magonjwa haya kuingizwa kwenye mitaala ya elimu ili wanafunzi wapate elimu ya awali kama ilivyo kwa HIV.
Aidha, Jafo aliwapongeza waandhaaji wa madhimisho hayo kwa kazi ya kuwafundisha walimu 40 ambao wamepewa mafunzo ya namna ya kutoa huduma kwa wananfunzi wenye ugonjwa wa pumu na kushauri toa mafunzi kwa walimu wa walimu na kushauri wigo wa kufundisha walimu hao kuo
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Magonjwa ya Mfumo wa Hewa (TARD) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukuzia(Tancida), Dk Digina Riwa alisema takwimu za WHO zinaonesha dunia inawagonjwa zaidi ya milioni 3 huku nusu ya wagonjwa hao ni watoto.
Alisema kwa Tanzania tawkimu hizo zinaoneshwa kuwa vifo 2,491 vinatokana na ugonjwa wa pumu na kuwa kutokana na makadirio ya kuwa wagonjwa wa pumu wanaweza kuongezeka kwa asilimia 30, Shirikisho hilo likajikita katika kutoa elimu.
Akizungumzia sababu ya maadhimisho hayo jiji Dodoma, Riwa alisema ni baada ya kubaniki kuwapo kwa tatizo hilo na kutoa takwimu kuwa kwa mwaka jana pekee wilaiaya ya Mpwapwa ilikuwa na wagonjwa 1,223, Kongwa ni 1,101, Chemba ni 1,459 na Chamwino wagonjwa 1512.
Alisema katika kuadhimisha mwaka huu wameamua kufanya upimaji katika shule za msingi na sekondari ambao wameweza kuwapata wale ambao wanajitambua kuwa na ugonjwa, lakini idadi kubwa ya wanafunzi walikuwa wahajitambui.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bahi na ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mwanahamisi Mukunda alihidi kuwa mkoa utaedeleza mkakati wa kutambua na kubaini watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa pumu.
“ Kwetu sisi mmetusaidia kubaini ukubwa wa tatizo, tumekuwa hatufanyi vizuri kwenye ufaulu kwenye mitihani ya taifa na tulikuwa tunatafuta mchawi, kumbe mmoja wa mchawi ni tatizo la pumu ambalo linachangia wanafunzi kukosa masomo.”alisema
0 comments:
Post a Comment