Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao umetengeneza mfumo wa matumizi ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi Serikalini.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa usikivu Taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari, leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao umetengeneza mfumo wa matumizi ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi Serikalini.
Sehemu ya wafanyakazi wa Wakala wa Serikali Mtandao wakifuatilia taarifa ambayo ilikuwa inatolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari, leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
Picha na Alex Sonna-Fullshangwe blog
WAKALA wa Serikali Mtandao umetengeneza Mfumo Shirikishi wa Kusimamia Shughuli na Rasilimali za Taasisi (ERMS) utakaowezesha kusimamia, kufuatilia, kukagua na tathmini ya utekelezaji wa shughuli zote za umma kwa ufanisi.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dk. Jabiri Bakari,wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dodoma amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa matumizi ya tehama katika kuboresha utendajikazi serikalini.
Dk.Bakari amesema kuwa wameamua kutumia utaalamu wetu wa kidigitali kutengeneza mfumo wa ERMS ambao ni dirisha moja linalounganisha shughuli zote za ndani ya taasisi kuongeza ufanisi katika utendajikazi na utoaji huduma bora kwa umma.
Aidha amesema kuwa kuwa mfumo huo utakuwa na moduli 18 zinazounganisha shughuli mbalimbali za utendajikazi zinazotegemeana kuwezesha kubadilisha taarifa miongoni mwa idara na kusimamia rasilimali watu, fedha na vitendea kazi.
Dk.Bakari amesisitiza kuwa mfumo huo unawezesha ushughulikiaji wa miamala kutoka idara moja hadi nyingine zikiwemo ankara za bidhaa na huduma, mapato na matumizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa shughuli kulingana na mipango na bajeti.
"Pia utawezesha usimamizi wa majukumu ya watumishi, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi, utekelezaji wa shughuli za manunuzi na utayarishaji wa taarifa mbalimbali za utendaji'',amesema Dk.Bakari
Hata hivyo amesema kuwa mfumo huu utawawezesha maofisa masuuli na watumiaji wengine wa mfumo kupata taarifa mbalimbali kulingana na mahitaji yao.
Dk. Bakari amesema kuwa mfumo huo wa ERMS unaweza kuunganishwa na kubadilishana taarifa na mifumo mingine mikuu ya serikali ikiwemo Mfumo Mkuu wa Uhasibu, Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Rasilimaliwatu (HCMIS), Mfumo wa Malipo ya Serikali Kieletroniki (GePG), Mfumo wa Barua pepe Serikalini (GMS) na Mfumo wa Ofisi Mtandao.
Pia amesisitiza kuwa moduli za mfumo huo zinaweza kuongezwa au kupunguzwa bila kuathiri utendaji kazi wa moduli nyingine au mfumo kwa ujumla.
Amezitaja baadhi ya mifumo mingine ambayo wakala umeitengeneza katika utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao ambao ni tovuti kuu ya serikali, tovuti kuu ya ajira, mfumo wa barua pepe serikalini ambao unatumiwa na taasisi za umma 402 zikiwemo ofisi za ubalozi nje ya nchi kwa ajili ya kubadilishana taarifa serikalini.
Aidha Dk. Bakari amezitaka taasisi za umma kuendelea kutumia tehama katika kuboresha utendaji kazi serikani na utoaji huduma kwa umma kwa kuzingatia miongozo na viwango vya serikani mtandao.
0 comments:
Post a Comment