Friday, 15 March 2019

Watu 49 wauawa kwenye shambulio la misikiti New Zealand

...
Watu 49 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch nchini New Zealand.

Kamishna wa polisi, Mike Bush amesema wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa wakihusishwa na tukio hilo huku akisisitiza kuwa huenda washukiwa wengine zaidi wakakamatwa.

Duru za habari zinasema washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali.

Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia. Amemtaja mshukiwa wa shambulio hilo kuwa "gaidi mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia".

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wameviambia vyombo vya habari kuwa walilazimika kutoroka kuokoa maisha yao na waliona watu walioanguka chini wanaovuja damu nje ya msikiti wa Al Noor.

Polisi inasisitiza kwamba hali bado haijaimarika na wamethibitisha pia kwamba "vilipuzi kadhaa vilivyofungwa kwenye gari vimeharibiwa".

Mwanamume wa Palestina ambaye alikuwa katika moja ya misikiti hiyo alisema aliona mtu akipigwa risasi kichwani.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger